Wednesday 23 March 2016

MKUU WA JESHI AUAWA KAMBINI..

Afisa mmoja muandamizi wa jeshi la Burundi, ameuwawa ndani ya makao makuu ya jeshi la Burundi.

Kanali Darius Ikurakure alikuwa Kamanda wa kambi ya kijeshi ya Muzinga, nje kidogo ya jiji la Bujumbura.
Kambi ya Muzinda iko kilomita 30 kutoka mji mkuu wa Bujumbura.
Kanali Ikurakure alikua msatari wa mbele katika harakati za kuzima maandamano na ghasia zilizotokea baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu mamlakani.

Duru kutoka kwa jeshi la burundi zinasema kuwa kanali huyo alipigwa risasi na mwanajeshi mwenza.

0 comments:

Post a Comment