Ni mwaka mmoja sasa umetimia tangu wasichana zaidi ya mia mbili walipotekwa nyara na kundi la Boko Haram la nchini Nigeria.
Wasichana hao walitekwa nyara tarehe na mwezi kama wa leo mwaka wa jana kutoka katika shule yao ya Chibok iliyoko katika jimbo la Borno.
Mpaka sasa haijajulikana hasa ni wapi walikofichwa wasichana hao,na tangu wakati huo kumekuwa na harakati zilizokuwa zikiendelea kushinikiza wasichana hapo waachiliwe kwa kauli mbiu ya Bring Back Our Girl kampeni ambayo imesambaa ulimwengu mzima,na sasa ulimwengu unawakumbuka wasichana hao leo tunapoadhimisha mwaka mmoja tangu kutoweka kwao.
Na kampeni hizi lengo na nia yake ni kuukumbusha ulimwengu kuwa, wasichana hao zaidi ya mia mbili bado wako kizuizini kwa mwaka mmoja sasa.
Kiwale 11blog imeinasa sauti ya Mkaazi wa jiji la Lagos nchini humo Judith Mwikali,akielezea kuhusiana na taarifa za kuonekana kwa mabinti hao upande wa kaskazini mwa nchi hiyo je taarifa hizo zina ukweli wowote ? msikie hapa chini Bi Judith anaeleza.
Insert 4-Judith
0 comments:
Post a Comment