Friday 17 April 2015

Ashtakiwa kwa kumtia mimba mwanawe…!!!!.

Mahakama moja mjini Bungoma nchini Kenya, imemshtaki afisa mmoja wa wadi ya Bukembe kwa kulala na mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka 14
kwa zaidi ya miaka miwili baada ya mkewe kufariki mwaka 2013.
Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya, mwathiriwa ambaye ni mjamzito wa miezi minne amesema kuwa mshukiwa huyo ambaye ni babaake,amekuwa akimlazimisha kufanya mapenzi naye kila usiku na kumuonya kwamba angemdhuru iwapo angemwambia mtu yeyote.
Binti huyo amesema kuwa Baba yake huyo pia ameninyima fursa ya kwenda katika shule ya upili licha ya kufanya vyema katika mtihani wa KCPE.
Amesema mwaka 2013 alifanya vyema lakini akanilazimisha kurudia darasa,na mwaka jana alifanya vizuri zaidi lakini anadhani kwamba iwapo atajiunga na shule ya upili ya bweni,baba yake atamkosa fursa ya kufanya tendo la ngono nay eye.
Hakimu mwandamizi Peter Ireri alimwachilia mtuhumiwa kwa dhamana ya shilingi laki moja ama pesa taslimu shilingi elfu ishirini.

0 comments:

Post a Comment