Spika wa Bunge Anne Makinda katika
kikao cha Bunge asubuhi ya leo, amelazimika kusitisha kikao cha bunge kwa muda
usiojulikana,kufuatia
mtarafuku uliosababishwa na miongozo juu ya suala la kura
ya maoni kwa katiba inayopendekezwa.
Mzozo ilianza pale mbunge wa Ubungo
Mheshimiwa John Mnyika , kuomba mwongozo,akihitaji swala la kura ya maoni
kujadiliwa leo hii kabla ya kutolewa majibu na serikali,kutokana na changamoto
kadha wa kadha ambazo zimekuwa zikijitokeza katika zoezi zima la uandikishwaji
katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Licha ya spika wa Bunge kutaka
serikali ilitolee ufafanuzi suala hilo pindi waziri mkuu atakaposimama
kuahirisha bunge,wabunge wa upinzani waliendelea kusimama na kushinikiza
kutolewa kwa kauli ya serikali.
Hebu sikia hapa jinsi sinema hiyo
ilivyokuwa huko bungeni mjini Dodoma.
Insert 1-Mzozo Bungeni
0 comments:
Post a Comment