Tuesday 28 April 2015

Kesi ya ndoa za jinsia moja kusikizwa US……

Harusi ya wapenzi wa jinsia moja


Mahakama kuu nchini Marekani hii leo inasikiliza kesi kadha, kuamua ikiwa wapenzi wa jinsia moja wana haki ya kisheria kuweza kufunga ndoa.

Suala hilo limeigawa Marekani kwa muongo mmoja uliopita, huku majimbo 36 kati ya majimbo yote 50 nchini humo yakiwa yamehalalisha ndoa za watu wa jinsia moja.
Mahakama itasikiliza rufaa kutoka kwa watu 16 kutoka majimbo manne ya Ohio, Michigan, Tennessee na Kentucky, ambapo ndoa hiyo bado ni haramu.
Ikiwa mahakama kuu itahalalisha ndoa hiyo, basi itakuwa halali kwenye majimbo yote 13 ambayo yamepiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.

0 comments:

Post a Comment