Friday 17 April 2015

Mapacha 5 wa kwanza kuzaliwa Marekani..!!!



Mapacha watano wa kike wamezaliwa Marekani katika hospitali moja ya wanawake mjini Texas Houston.

Wauguzi katika hospitali hiyo wanasema kuwa uzazi huo kutokana na mimba moja ni rekodi mpya, ambayo haijawahi kutokea Marekani.
Danielle Busby ambaye ndiye mama wa watoto hao ambao wamepewa majina ya Olivia Marie, Ava Lane, Hazel Grace, Parker Kate na Riley Paige,anasema kupata watoto hao wote wakiwa wazima kwake ni baraka ya hali ya juu.


Inasemekana watoto wengi sawa na hao walihahi kuzaliwa mara moja huko London Uingereza, mwaka 1969 katika hospitali ya Queen Charlotte.

Zaidi ya Madaktari na wauguzi 12 walilazimika kufanya kazi ya ziada ilikumsaidia bi Busby kujifungua watoto hao, ambao hawakuwa wametimiza umri wa miezi tisa tumboni kwa njia ya upasuaji .
Baba wa mtoto huyo Adam Busby amewamiminia sifa kedede wahudumu wote wa hospitali hiyo waliofanikisha operesheni hiyo.
Bwana Busby amesema kuwa mwanawao wa kwanza Blayke anawasubiri kwa hamu na ghamu, kwaona ndugu zake hao.
Bi.Busby alikuwa na tatizo la kupata ujauzito hivyo akatumia mbegu pandikizi ya uzazi kwa mimba zake zote mbili.

0 comments:

Post a Comment