Wednesday 22 April 2015

Hii ni rekodi ya mpangaji kukaa muda mrefu kwenye nyumba moja....



Hii sio mbali sana, inatokea mtaa wa Old Ngara, Kenya ambako kuna mzee mmoja ambae ameishi kwenye nyumba kwa muda mrefu,zaidi inaweza kuwa rekodi mpya sababu sikuwahi kuisikia kwingine
.
Mzee huyo Adam Mamuji amesema ameishi kwenye nyumba hiyo tangu mwaka 1944 kabla nchi hiyo haijapata uhuru, wakati huo alikuwa akiishi na wazazi wake ambao walifariki,kipindi hicho kodi ilikuwa shilingi 45 za Kenya.
Mzee Adam amesema mwaka 1948 kodi ilipanda na kufikia shilingi 140, lakini kwa sasa wanalipa shilingi elfu 10 za Kenya.
Amesema hawezi kutafuta nyumba nyingine tena kwa sababu ameishi kwa muda mrefu kwenye nyumba hiyo ameiomba Serikali imuuzie.
Nimeamini hakuna watu watunzaji wa vitu kama wazee, huyu mzee ametoa mpaka risiti ya Kodi ya nyumba aliyolipia miaka ya 1940 !!
Hii story yote nimekuwekea hapa chini  kwenye video,ambayo iliripotiwa na kituo cha K24 Kenya.


0 comments:

Post a Comment