Tuesday 28 April 2015

Mahakama Kuu Kenya yabariki chama cha mashoga!!!!



Katika hatua ya kushitua Mahakama Kuu nchini Kenya, imesalimu amri mbele ya mashinikizo ya watetezi wa vitendo vichafu vya ulawiti na usagaji,
na kusema kuwa sasa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uasherati wanaweza kusajili mashirika ya kile kinachodaiwa ni kutetea haki zao za kibinadamu.

Majaji watatu wa mahakama hiyo wameiamuru Bodi ya Kusimamia Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs), kulitambua na kulisajili shirika moja ambalo awali mahakama hiyo ilizuia lisisajiliwe kwa sababu za kimaadili na kidini.

Jopo hilo la majaji Isaac Lenaola, Mumbi Ngungi na George Odunga limedai kuwa, katiba ndio marejeo ya kila kitu nchini Kenya na kwamba serikali haitakiwi kuzingatia mafundisho ya kidini katika maamuzi yake ambayo kwa mujibu wa majaji hao, maamuzi hayo yananyima kundi fulani la watu uhuru wao.

Hatua ya Mahakama Kuu ya Kenya imechukuliwa pia katika wakati huu wa kukaribia ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini Kenya, ambaye ni mtetezi mkuu wa vitendo hivyo vichafu.

0 comments:

Post a Comment