Friday 17 April 2015

Story Hot Magazetini leo April 17-2015

Hizi ndizo story zilizopamba kurasa za mbele kwenye Magazeti mengi leo April 17-2015.
Dereva aliyebeba watuhumiwa wanaodaiwa kuwa magaidi huko Kidatu asimulia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Magesa Mulongo amesema taarifa za magaidi kuvamia
mkoa huo sio za kweli, Mtanzania abuni kifaa cha kufundishia bila mwalimu, Mkurugenzi wa TEHAMA, Ally Simba amesema sheria za usalama wa mitandao zilizowasilishwa Bungeni hivi karibuni zimetungwa kukidhi matakwa ya kimataifa, Jeshi la Polisi Dar limeanza kuimarisha usalama katika maeneo hatarishi kwa kufanya doria..
Nyingine ni kuhusu binti anaedaiwa kubakwa na Emmanuel Mbasha vipimo vimeonyesha hakufanyiwa kitendo hicho,  Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amejikuta kwenye wakati mgumu wakati akizungumza na wananchi wa jimbo lake, Waziri Samuel Sitta amemsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya reli Kapallo Kisamfu na Wanafunzi wa shule ya Tusiime wameendelea kufanya vizuri baada ya shule yao kupewa Tuzo.


0 comments:

Post a Comment