Wakazi
wa jimbo la South Carolina nchini Marekani waliandamana jana kulaani mauaji ya
dereva mweusi aliyepigwa risasi na kuuawa na polisi mzungu.
Waandamanaji hao ambao wengi wao walikuwa Wamarekani wenye asili ya Afrika,wameonesha kusikitishwa na mauaji hayo ambayo wanasema yamefanyika kwa sababu za kibaguzi.
Dereva
huyo alipigwa risasi na polisi barabarani baada ya kutokea mabishano baina ya
wawili hao.
Mkanda
wa video wa mauaji hayo unamuonesha polisi Michael Slager akimpiga risasi 8
mgongoni dereva huyo,huku akijaribu kukimbia.
Kesi ya
Scott imezusha tena mjadala mkubwa nchini Marekani kuhusu mauaji yanayofanywa
na polisi wazungu wa nchi hiyo dhidi ya raia weusi
0 comments:
Post a Comment