Thursday 9 April 2015

Mume Apewa Talaka kupitia facebook..!!!!

Hii inatokea huko nchini Ghana,mwanaume mmoja amepewa talaka na mkewe kupitia mtandao wa kijamii Facebook.

Talaka hiyo ilitolewa baada ya mkewe kuenda mahakamani akidai kuwa,haki zake za unyumba zimekiukwa na mumewe ambaye hataki kuonekana nyumbani.
Mwanamke huyo mkaazi wa jiji la Brooklyn alitaka ruhusa ya mahakama kubadilisha hali yake ya ndoa kuwa “single” kwenye Facebook.
Jaji wa mahakama hiyo ya rufaa ya Manhattan Matthew Cooper, aliamua kuwa mwanamke huyo muuguzi Ellanora Baidoo anaweza kumtaliki mumewe kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Baidoo 26 ameruhusiwa kutangaza talaka yake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook,kwa sababu ndio njia ya pekee ambaye anawasiliana na mumewe.
Na mara moja wakili wake mwanamke huyo alituma ujumbe wa kibinafsi kwa Victor Sena Blood-Dzraku akimjulisha kuhusu talaka hiyo.
Mwana Mama huyo alifunga ndoa na mshtakiwa Blood-Dzraku mwaka wa 2009 lakini ndoa yao ilisambaratika Blood-Dzraku alipokataa kata kata kuendelea mbele na sherehe za kitamaduni kuambatana na mila za Bi Baidoo.
Bibi huyo amesema kuwa hataki kulipwa fidia yeyote kutoka kwa mumewe kwani japo walifunga ndoa mumewe alikataa kutimiza tendo la ndoa naye.
Aidha majaribio kadha ya kuwapatanisha wawili hao imeambulia patupu huku ikibainika kuwa bwana Blood-Dzraku hataki kutoa talaka.
Kulingana na wakili huyo wa Bi Baidoo,amesema bwana huyo hajajibu ujumbe huo wa talaka,aliotumiwa katika ukurasa wake wa facebook.

0 comments:

Post a Comment