Ugiriki inatarajiwa leo Alhamisi kulipa nusu ya deni lake la dola milioni 450 inayodaiwa na shirika la fedha Duniani IMF.
Kuna wasiwasi iwapo serikali ya Ugiriki itapata fedha hizo na kulipa, lakini waziri wa Fedha Yanis Varoufakis, ametangaza hadharani kuwa Athens itatimiza ahadi yake.
Ugiriki inataka mikopo zaidi, huku madeni mengine yakilipwa ilihali pia taharuki inaongezeka kutoka kwa umma ambao hawajalipwa fedha zao za malipo ya uzeeni na za kustaafu
0 comments:
Post a Comment