Tuesday 21 April 2015

Rais wa zamani Misri ahukumiwa miaka 20 gerezani!!!

Rais wa zamani Mohammed Morsi
Makahama nchini Mirsi imemhukumu aliyekuwa rais wa zamani Mohammed Mosri kifungo cha miaka 20 gerezani kutokana na kuuawa kwa waamdamanaji wakati akiwa madarakani.

Hii nidyo hukumu ya kwanza kutolewa kwa Morsi tangu aondolewe madarakani, na moja moja ya hukumu zinazomuandama.
Mosri aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake.
Wafuasi wa Morsi 
Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya rais mwishoni mwa mwaka 2012.
Wakati umati ulipokusanyika nje ya ikulu bwana Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo.
Baadaye Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa kwenye makabiliano, wengi kutoka kwa Muslim Brotherhood.
Kabla ya kutolewa hukumu ya leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha.
>>>>Bbc

0 comments:

Post a Comment