Thursday 30 April 2015

Uuzaji holela wa Antibayotiki moja ya sababu za usugu kwa tiba:WHO

Usugu wa dawa aina ya viuavijisumu au antibayotiki kwa magonjwa umesalia kuwa changamoto
kubwa kwa nchi nyingi ulimwenguni na hivyo kukwamisha harakati dhidi ya magonjwa, imesema ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO iliyotolewa leo.
Ripoti hiyo inafuatia utafiti ulioshirikisha serikali kwenye nchi 133 wanachama wa shirika hilo ambapo imebaini mambo makuu matano ikiwemo nchi 34 kati ya zilizoshiriki ndizo zenye mipango ya kitaifa ya kudhibiti usugu wa dawa hizo, uhaba wa maabara thabiti za kufuatilia usugu wa madawa na uuzuaji holela wa dawa hizo bila kibali cha daktari.
Halikadhalika ripoti imetaja suala la dawa zisizokidhi viwango,ukosefu wa miongozo ya matumizi yake na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu athari za matumizi ya dawa hizo.
 Nchi Nane kati ya 47 za Afrika ambazo zilishiriki utafiti huo zimesema usugu wa antibayotiki ni changamoto kubwa katika tiba dhidi ya Malaria na Kifua kikuu halikadhalika uduni wa ubora wa dawa hizo.

0 comments:

Post a Comment