Friday 24 April 2015

Itizame hapa Ratiba ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

Hatimaye wanafunzi wa zamani wa kocha wa Manchester United Louis Van Gaal, katika klabu ya FC Barcelona watapata nafasi ya kuonyeshana umwamba katika kuelekea jijini Berlin Ujerumani ambapo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya itachezwa. Ratiba ya nusu fainali ya michuano hiyo imepangwa muda mfupi uliopita huko Nyon Uswiss.
Ratiba inaonyesha Luis Enrique ataiongoza FC Barcelona kukupiga dhidi ya FC Bayern Munich inayofundishwa na mchezaji mwenzie wa zamani wa Barca Pep Guardiola.
Guardiola na Luis Enrique walikuwa kwenye kikosi kimoja cha Barca kilichokuwa kikifundishwa na Van Gaal msimu wa 1999/2000.
Kwa upande mwingine mabingwa watetezi wa kombe hilo Real Madrid, watacheza dhidi ya Juventus.
Mechi za raundi ya kwanza zitachezwa Mei 5 na 6 na marudiano zitakuwa wiki moja itakayofuatia ya tarehe 12 na 13.

0 comments:

Post a Comment