Thursday 16 April 2015

Milipuko hatari yanaswa msikitini Morogoro..!!!!


Polisi mkoani Morogoro imewatia mbaroni watu zaidi ya tisa wanaojihusisha na uhalifu wakiwa na milipuko hatari na zana za milipuko,
wakiwa wamefichwa ndani ya Msikiti wa Suni kata ya Kidatu, wilayani Kilombero, mkoani Morogoro.
Licha ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, mwingine ameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira baada ya kumshambulia na kumkata kwa jambia shingoni askari polisi mwenye namba F. 3323 Koplo Nassoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo,amethibitisha jana na kusema watu hao walikamatwa juzi majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha Nyandeo, Kijiji cha Chicago, kata na tarafa ya Kidatu, wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Hata hivyo amesema Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba uongozi wa msikiti kuwatoa watu wote waliokuwa msikitini,ili kuweza kubaini watu ambao wanatiliwa mashaka.
Kiwale 11 blog ilimtafuta kamanda wa Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo na kupiga nae story kutaka kujua kuhusiana na tukio hilo,na je ni kweli kuwa waliokamatwa ni wanachama wa Al Shaabab,karibu usikie mahojiano hapa chini.




0 comments:

Post a Comment