Tuesday 14 April 2015

Bibi wa umri wa miaka 65 ana ujauzito wa pacha wanne..!!!!!

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 kutoka Berlin Ujerumani ambaye ana watoto kumi na watatu, ametangaza kuwa ni mja mzito na Mapacha wanne.

Kwa mwaka mmoja na nusu sasa Bi:Annegret Raunigk ambaye ni mwalimu wa kingereza na kirusi,amekuwa akijaribu kupata mtoto mwingine kwa njia ya upandikizaji,kulingana na vyombo vya habari vya German RTL.
Bibi huyo anasema kuwa alilazimika kuwatafuta watoto zaidi baada ya kitinda mimba wake mwenye umri wa miaka 9 kumsihi kumtafutia watoto atakaocheza nao.
Bi Raunigk ambaye amebeba ujauzito huo kwa majuma 21 sasa, anasema kuwa alishtuka kujua kuwa alikuwa amejaaliwa ujauzito wa watoto 4 wala sio mmoja kama alivyotarajiwa.
Bi Raunigk aliyechangiwa mayai na mbegu za kiume, anawatoto wengine 13 kutoka kwa baba watano tofauti.
Aidha mwanawe Leila alizua mjadala mkali alipozaliwa mwaka wa 2005 lakini hilo halimsumbui bibi huyo, ambaye mwanawe wa kwanza ana miaka 44.
Mahojiano ya bibi huyo na runinga hiyo ya kijerumani yamevuta hisia nyingi za watu yalipopopeperushwa hewani.
Mbali na kufurahiwa wanawe 13 Bi Raunigk anawajukuu 7,na kufikia sasa mimba hii ya kihistoria haijaonesha hitilafu yeyote.
Kufikia sasa mwanamke anayeshikilia rekodi duniniani ya kuwa mama aliyejifungua pacha wanne ni Merryl Fudel,aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 55.
Vilevile mwanamke ambaye anashikilia rekodi ya kujifungua akiwa na umri mkubwa zaidi ni Omkari Panwar kutoka India, aliyejifungua akiwa na miaka 70.

0 comments:

Post a Comment