Wednesday 22 April 2015

Adhabu ya Viboko yasababisha kifo cha mwanafunzi...!!!!!!




Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari ya Matui iliyopo Wilayani Kiteto, Mkoani Manyara Emmanuel Mbigima mwenye miaka 15,amefariki dunia
baada ya kuchapwa viboko 12 na walimu wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Christopher Fulme,amesema mwanafunzi huyo alifariki dunia baada ya kuchapwa viboko na walimu wake watatu kutokana na kufeli somo la Kiswahili.
Mauaji hayo yalitokea juzi saa 4 asubuhi shuleni hapo na mwili wake kwa sasa unaendelea na uchunguzi.
Msemaji wa familia Emmanuel Ngowi, amesema familia inataka kuona haki inatendeka juu ya kifo chandugu yao.
Chama cha Walimu Kiteto kimelaani tukio hilo na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kujua ukweli kuhusu kifo cha mwanafunzi huyo.
Hata hivyo baada ya taarifa hizo kuzagaa mitaani kundi la wananchi wenye hasira kali walivamia kituo cha Polisi kwa lengo la kulipiza kisasi kwa kutaka kuwaua walimu hao.

0 comments:

Post a Comment