Tuesday 14 April 2015

Baaada shambulio Chuo Kikuu Garissa,Kenya yafanya maamuzi Magumu!!!!


Familia za wanafunzi 142 kati ya  148 waliouawa katika shambulio la kigaidi la Al Shabaab kwenye Chuo cha Garissa Kenya
wameruhusiwa kuchukua miili ya ndugu zao kwa ajili ya mazishi ambapo Serikali ililazimika kutumia mashine maalum kutambua baadhi ya miili ambayo iliharibika vibaya kutokana na majeraha ya risasi.
Lakini bado kuna jambo lililotata kwani zaidi ya wanafunzi 166 hawajulikani walipo,na familia zao bado zimeendelea kulalamika kutokana na baadhi ya ndugu zao kutoonekana.
Jambo jingine linaliripotiwa kutoka huko ni kwamba Uamuzi mgumu umechukuliwa,baada kenya kulitaka Shirika la Wakimbizi UNHCR ndani ya miezi mitatu kufunga kambi ya wakimbizi,iliyoko mashariki mwa nchini hiyo pamoja na kuwarudisha kwao wakimbizi ambao ni raia wa Somalia zaidi ya laki nne.
Sikiliza Taarifa kamili hapa chini iliyoriotiwa na kituo cha K24 nchini humo.




0 comments:

Post a Comment