Friday 17 April 2015

Kwanini wanaume wanajitoa uhai ? Soma utafiti……



Wanaume wengi wenye umri kati ya miaka arobaini na 50 wamo katika hatari kubwa ya kujiua kuliko wanawake.

Kijana mmoja kutoka Uingereza Simon Jack, alifanya utafiti huo baada ya baba yake kujiua katika siku yake ya kuzaliwa miaka 25 iliyopita akiwa na umri wa miaka 44.
Jack anasema alianza kuwa mdadisi kwa simulizi zote au habari kuhusu watu wanaojiua na amegundua kuwa wote ni wanaume.



Sikujua kuwa kujiua ni adui mkubwa wa watu wenye umri chini ya miaka 50,ila sasa nafahamu kwanini wanaume mia moja wamejiua ndani ya wiki''.
Idadi hiyo imekuwa kubwa zaidi kuliko wakati wowote katika miaka 14 iliyopita ya wanaume wanaomaliza maisha yao wenyewe ni mara nne ya wanawake.
Jack alitamani kufahamu sababu inayowafanya wanaume kufanya matukio hayo zaidi.
Na kama kuna namna yeyote ya kuzuia mauaji haya, ''Nilijiuliza nini kinachopelekea wanaume hawa kufanya hivi?
Miaka 40 ni miaka ambayo mtu ana majukumu mengi, Unaweza kudhani kuwa mke wake amemuacha na kuchukua watoto wote,au kapoteza kazi yake katika umri huo wakati ni vigumu kupata mwingine''alihoji Jack.
''Au sababu yoyote ambayo inaweza kumpa shinikizo mwanaume ambaye anahitajika kuhudumia familia yake''.
Kwa upande wa baba yake Jack, haikuwa hivyo kwani alikuwa ni baba mzuri mwenye upendo kwa familia yake,mwenye uwezo na umaarufu.
Kila mtu atakubali kuwa ni tatizo kubwa katika familia pale unapompoteza mtu kwa sababu ya ugumu wa maisha uliokithiri au kuachwa na mpendwa wako.
Wengine walitoa maoni kuwa wengi wanaojiua ni ushahidi tosha kuwa wana matatizo ya kiakili au wana msongo wa mawazo au huzuni katika maisha.
Prof Rory O'Connor ambaye anaongoza kituo maarufu duniani cha utafiti katika chuo kikuu cha Glasgow,anasema tabia ya kujuiua ni tatizo la kisaikolojia ambalo hutokana na upungufu wa kiakili.
Ingawa watu wenye matatizo ya akili uwa ni vigumu sana kujiua ni asilimia tano tu ndio wanaweza kujiua kutokana na upungufu wa akili.
Hata hivyo katika maamuzi kuna tofauti kubwa kati ya namna wanaume na wanawake wanavyo weza kujielezea matatizo yao na kuyatatua.
''wanawake huwa wanatumia njia za kujieleza ambazo ni rahisi watu kumuokoa tofauti na wanaume''
Jack anasema ”Natamani kujua nini kilimpata baba yangu kwani fumbo hili linaweza jibu maswali ya familia nyingi wenye matatizo kama yangu”.


0 comments:

Post a Comment