Monday 20 April 2015

Mayunga toka Tanzania ndio mshindi wa Airtel TRACE Music STARS!!!!

Majaji wakifuatilia waimbaji kushoto ni Akon


Fainali ya shindano hilo ilikua ni Jumamosi ya April 18 2015 ambapo shindano la Airtel Trace Music
Stars lilifanyika Nairobi Kenya likiwa ni shindano la kumtafuta mkali wa kuimba ambapo zilishirikishwa nchi 13 kutoka Afrika na Mtanzania Nalimi Mayunga ndio akashinda.
Super star huyu mpya amezaliwa ambapo miongoni mwa vitu atakavyovifanya ni kuungana na Akon kwenye studio yake huko Marekani kwa ajili ya kurekodi single yake ya kwanza (Mayunga).

Mayunga kwenye fainali Nairobi, hii ilikua ni muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi.
Unaweza kusikiliza alivyoimba wimbo wa mwisho kabla ya kutangazwa mshindi kwa kubofya hapa chini.


0 comments:

Post a Comment