Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umesema umeanza utambuzi wa
Watanzania waishio katikmaeneo ya hatari nchini humo,kabla ya kuanza hatua za
kuwaondoa na kuwarejesha nyumbani.
Hatua hiyo inatokana na kushamiri kwa mashambulizi yanayofanywa na raia wa
Afrika Kusini dhidi ya raia wa kigeni,ambapo hadi kufikia jana watu sita
wameuawa.
Taarifa zilizopo hata hivyo zinasema kwamba hakuna raia wa Tanzania ambaye
ameuawa au kujeruhiwa katika vurumai hizo ambazo zimeanza Durban, Kwa- Zulu
Natal.
Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Mindi Kasiga, amesema kwamba Ubalozi Afrika Kusini umepeleka maofisa wake
katika mji wa Durban kuangalia hali ilivyo.
Kasiga amesema kwamba serikali imeshatoa mwongozo wa namna ya kuwaondoa raia
wake nchini Afrika Kusini.
Amesema kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, ambaye yuko nje kwa
safari ya kikazi atatoa taarifa mara tu atakapowasili nchini.
Kiwale 11 blog imezungumza na kaimu balozi wa Tanzania nchini humo Elibahati Lowassa, akieleza hali ilivyo mpaka sasa nchini humo,Bonyeza hapa chini kumsikia.
0 comments:
Post a Comment