Thursday, 30 April 2015

Askari wa Ufaransa wanajisi watoto CAR...

Mmoja wa wanajeshi wa Ufaransa
Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wanachunguza tuhuma za ngono kwa watoto zinazodaiwa kufanywa na wanajeshi wa nchi hiyo pindi walipokuwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wizara ya Ulinzi imesema itahitaji kutolewa kwa adhabu kali zaidi dhidi ya yeyote atakae patikana na hatia.
Mashtaka hayo yamefunguliwa baada ya kupatikana kwa nyaraka zilizotolewa mwezi July na mfanyakazi mwandamizi wa Umoja wa Mataifa.
Afisa huyo alisimamishwa kazi baada ya kupewa nyaraka hizo za siri kwa Ufaransa. Farhan Haq, msemaji msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon, amesema Umoja wa Mataifa umefanya uchunguzi wa tuhuma hizo, ambazo itazifuatilia kwa kina.

Related Posts:

  • Japan yakumbuka shambulio la Hiroshima… Raia wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima. Takriban watu laki moja na arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani… Read More
  • Usikose nakala yako ya gazeti la TABIBU kesho Alhamisi kwa bei ya sh. 500/= tu. … Read More
  • Utamaduni wa kurejesha mahari marufuku Uganda…… Ngombe hutumiwa sana kulipa mahari UgandaMahakama ya juu zaidi nchini Uganda imesema kuwa utamaduni wa kurejesha mahari baadaya talaka katika ndoa za kitamaduni unakiuka katiba na utamaduni huo unapaswa kupigwa marufuku. … Read More
  • Michuano ya dunia Mpira wa pete kuanza…. Michuano ya kumi na nne ya Kombe la dunia la mchezo wa pete itaanza kutimua vumbi leo katika jiji la Sydney nchini Australia. Jumla ya michezo sitini na minne itacheza katika siku kumi za michuano hiyo ambapo timu kumi n… Read More
  • Je unataka kuishi maisha marefu duniani…..? Utafiti mmoja uliofanywa nchini China,umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu. Utafiti huo haswa umeonesha kuwa ukila chakula hususan pilipili, utaishi maisha marefu zaidi duni… Read More

0 comments:

Post a Comment