Wednesday 1 April 2015

Tanzania yatengeneza printa ya aina yake..!!!

Huenda isiwe inafahamika na Watanzania wengi, lakini mashine ya kwanza ya kuchapa vifaa vya maumbo mbalimbali, imeanza kutengenezwa nchini.
Kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki na Kati, Printa inayochapa kitu katika pande tatu maarufu kwa kiingereza kama ‘3D Printer’, imetengenezwa jijini Dar es Salaam katika kituo cha kukuza ubunifu na ujasiriamali cha Buni Hub.
Printa hiyo yenye uwezo wa kutengeneza vifaa mbalimbali vya plastiki kutokana na usanifu wake, ilitengenezwa na timu ya wataalamu wa elektroniki na teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) baada ya kupatiwa ujuzi na mtaalamu kutoka Uingereza, Mathew Rogge.
Kwa wengi waliozoea printa za kuchapa karatasi watashangazwa na uwezo mkubwa wa printa hiyo inavyoweza kuuchapa mchoro uliopo kwenye kompyuta hadi kuwa kifaa pasina kukosea.
Baada ya wiki tatu za kuitengeneza, printa hiyo imeshatengeneza vifaa kadhaa vya plastiki vinavyoweza kutumika kama vipuri kutengenezea mashine nyingine ya namna hiyo.
Tofauti na printa zinazochapa karatasi ambazo hutumia wino kuchapa, printa za 3D zinatumia malighafi za plastiki, chuma, udongo, na nyinginezo ziitwazo ‘filament’ kuzalisha bidhaa tofauti kutokana na mahitaji.
Kuingia kwa teknolojia ya uundaji printa za 3D hasa kwa kutumia taka za kielektroniki, kutapunguza gharama za ununuzi wa mashine hizo zilizoanza kupata umaarufu ulimwenguni kwa kurahisisha kazi lukuki ambazo awali zilifanyika kiwandani.
Matumizi shuleni

0 comments:

Post a Comment