Tuesday, 27 February 2018

RAMAPHOSA ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI…

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ametangaza baraza lake jipya la mawaziri.
Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo.

Nene alifukuzwa Disemba 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.
Palipotokea anguko la thamani ya randi alilazimika kumfukuza Rooyen na kumchagua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia alimfukuza kazi siku za mbeleni.
Katika baraza la Ramaphosa Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara.
Aliyekuwa mke wake Zuma Nkosazana Dlamini-Zuma, ameteuliwa kuwa waziri wa ofisi wa rais.
Bw Ramaphosa ambaye ni mfanya biashara wa umri wa miaka 65, katika hotuba yake ya taifa awali mwezi huu, aliahidi kupambana na rushwa na kuboresha uchumi wa nchi hio.

Related Posts:

  • AHUKUMIWA KIFUNGO KWA KULALA NA MPENZI WA MWANAE… Mwanamke mmoja ambaye ametambulika kwa jina la Alaine Goodman (46) amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mapenzi na kijana mwenye umri mdogo ambaye ni mpenzi wa mtoto wake. G… Read More
  • SERIKALI: UZALISHAJI WA CHAKULA UTAFIKIA TANI MILIONI 3 Serikali imefanya tathmini ya awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini na kubaini kuwa uzalishaji wa chakula nchini utakuwa na ziada ya tani 3,013,515. Hayo yamesemwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles … Read More
  • EU: DONALD TRUMP NI TISHIO KWA ULAYA… Rais wa Baraza la muungano wa Ulaya Donald Tusk ameonya kwamba maamuzi ya kutia wasiwasi yanayofanywa na Donad Trump ni miongoni mwa chanagmoto zinazokumba muungano huo. Amesema kuwa mabadiliko yaliofanyika nchini Marek… Read More
  • MVUA YALETA MAAFA WILAYANI MPWAPWA… Watu wanne wakiwamo watatu wa familia moja ambao ni wakazi wa Kijiji cha Isighu kitongoji cha Majumba Sita wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wamekufa maji baada ya makazi yao kusombwa na mvua iliyo nyesha usiku wa kuamkia Ja… Read More
  • SUDAN YAPINGA AMRI YA TRUMP..! Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Sudan imemuita mwanabalozi wa Marekani mjini Khartoum kupinga hatua ya Rais Donald Trump ya kuwapiga marufuku raia wa nchi hiyo kuingia Marekani. Sudan inasema kuwa hatua hiyo… Read More

0 comments:

Post a Comment