Tuesday 27 February 2018

WAKUU WA MAJESHI WAFUTWA SAUDI ARABIA………..

Saudi Arabia imewafuata makamanda wa vyeo vya juu jeshini, akiwemo mkuu wa majeshi.
Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa makanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.

Taarifa hizo zilichapishwa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia la SPA, lakini hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa makamanda hao.
Mrithi wa ufalame Mohammed bin Salman, ambaye pia ni waziri wa ulinzi anaaminiwa kuhusika kwenye mabadiliko hayo.

Mwaka uliopita watu mashuhuri nchini Saudi Arabia wakiwemo wanawafalme, mawaziri na wafanyabiashara matajiri, walifungiwa kwenye hoteli ya kifahari ya Ritz-Carlto, wakati mwanamfalme huyo aliongoza mikakati dhidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka.

0 comments:

Post a Comment