Tuesday 27 February 2018

NYOKA MWENYE SUMU KALI AGUNDULIWA NDANI YA MKEBE WA CHAKULA CHA MTOTO AUSTRALIA……….

Mwanamke amegundua nyoka mwenye sumu kali ndani ya mkebe ambao mtoto wake anatumia kebeba chakula cha mchana nchini Australia.

Nyoka huyo aligunduliwa amejificha kwenye kifuniko, wakati mama huyo alikuwa akiweka chakula kwenye mkebe huko Adelaide, kulingana mshikaji nyoka Rolly Burrel.
Bw Burrel alisema almshauri mwanamke huyo kufunika mkebe na kuupeleka nje wakati alimpigi simu kumuomba usaidizi.
Alimtaja nyoka huyo kama eastern brown, mmoja wa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani,na alisema nyoka huyo alitolewa salama.
Mshikaji nyoka huyo alisema kuwa anashuku nyoka huyo aliiangia kwennye mkebe huo kwa sababu labda ndiko alipata giza.

Nyoka wa aina hiyo hupatikana maeneo ya pwani mwa Australia na amehusika na vifo 23 tangu mwaka 2000 kwa mujibu wa utafiti.

0 comments:

Post a Comment