Thursday 18 October 2012

Je wajua kicheko ni Tiba ya Ukweli?

Utafiti umeonyesha kwamba faida ya kucheka ni kubwa na inayofaa kwa afya ya mwili na akili. Watafiti hadi sasa wamedokeza kuwa kicheko husaidia kupunguza maumivu, kuleta furaha zaidi, na hata kuongeza kinga. Kicheko kwa hiyo, ni dawa isiyo na gharama ambayo kila mmoja anaweza kuipata. Kinachotakiwa ni kujenga mazoea ya kufurahi na kujitahidi kuwa na hisia ya ucheshi mara kwa mara. Faida za kicheko: 1.Homoni: Kicheko hupunguza kiwango cha homoni zinazoleta msongo(stress) kama cortisol na epinephrine dopamine (Adrenaline). Pia huongeza kiwango cha homoni ya kuimarisha afya kama endorphins na neurotransmitters. Kicheko husababisha kuongezeka kwa idadi ya seli za kinga (antibody); pia huzalisha na huongeza ufanisi wa seli T. Yote hii ina maana kuwa mfumo wa kinga mwilini huimarika, na hupunguza uwezekano wa msongo wa mawazo(Stress). 2.Mwili kujiachia(Physical release): Baada ya kicheko akili na mwili hupata hisia nzuri, ni kama unajiachia 3.Utendaji wa ndani Kicheko hutoa mazoezi ya kiwambo (diaphragm), husaidia mabega (works out the shoulders) na kufanya misuli kushirikiana zaidi;lakini pia husaidia moyo(provides a good workout for the heart). Kicheko pia huondoa hasira, hatia, dhiki na hisia hasi. 4.Kijamii Kicheko hutuunganisha na wengine. Kucheka hujenga mahusiano mema na huleta kuaminiana.Furaha na faida ya kicheko huongezeka maradufu ikiwa watu wengi wanacheka pamoja.Kicheko ni njia nzuri ya kufahamiana na kushirikiana. Unaweza je kucheka: Kicheko ni moja ya tiba mbadala ya bure, urahisi na yenye manufaa kwa njia nyingi. Unaweza kupata zaidi kicheko katika maisha yako kwa mikakati ya ifuatayo: 1.Angalia vipindi vya TV vya kuchekesha pamoja na filamu za ucheshi. 2.Cheka na marafiki kazini,shuleni na hata nyumbani. Fanya kicheko kuwa tabia yako. 3.Acha kulalamika kuhusu maisha,jaribu kucheka. Kama jambo fulani linakuchanganya ni vizuri kuangalia nyuma juu yake na kucheka. Usikubali kusongwa na mawazo,zungumza na wenzako lakini juu ya yote angalia,soma au kumbuka mambo yatakayokuchekesha ! Wachaaaa nichekeeee mieeeee Haaahaaaa ahaaaaaaa....Yeeaaaaaahhh

0 comments:

Post a Comment