Monday, 5 November 2012

HEBU TAFAKARI HAYA KWA KINAaaaa.....

1. Maisha yako yanaweza kubadilishwa kwa muda mfupi na mtu hata usiemjua. 2. Watu wenye furaha pengine hawana kila kitu cha kuwapa furaha ila kile kidogo walichonacho hukipa maana ya kukifurahia.3. Wapenzi wawili wanapogombana haimaanishi hawapendani,vivyohivyo wasiogombana haimaanishi wanapendana. 4. Unaweza kufanya jambo fulani la muda mfupi lakini likakunyima furaha milele .5. Unapoagana na uwapendao waache na maneno mazuri pengine inaweza kuwa mara yako ya mwisho kuwaona. 6. Inaruhusiwa kuwa na hasira ila haimaanishi uwe katili.7. Ukomavu wa mtu huja kutokana na changamoto alizozipitia kwenye maisha na kujifunza kupitia changamoto hizo na sio umri aliouongeza. 8. Wakati mwingine inatosha kusamehewa na wengine,ifike mahali ujifunze kujisamehe mwenyewe. 9. Sio lazima uwe na kiherehere cha kujua siri flani pengine kuijua kunaweza kubadili maisha yako milele. 10. Watu wawili wanaweza kutazama kitu kimoja lakini kila mmoja akaona tofauti

Related Posts:

  • Usikose kusoma gazeti la TABIBU kesho alhamisi likiwa limesheheni habari mbalimbali kuhusu afya. Ni kwa bei ya sh. 500/= !!                             … Read More
  • Pombe kidogo pia yaweza kuleta saratani……….. Unywaji kidogo wa pombe hadi chupa moja kwa siku kwa wanawake na chupa mbili kwa wanaume, unaweza kusababisha hatari ya kupata saratani kulingana na watafiti. Makala moja ya Uingereza ilichambua utafiti mkubwa kutoka nch… Read More
  • Juma Kaseja ajiunga na Mbeya City…… Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu bila timu, golikipa mkongwe na mahiri Juma Kaseja August 19 amesaini mkataba wa miezi sita wa kuitumikia klabu yaMbeya City kutoka Jijini Mbeya. Mkataba wa … Read More
  • Kufanya kazi kwa saa nyingi ni hatari…… Utafiti uliofanywa kwa zaidi ya watu laki tano, umeeleza kuwa watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi, wako hatarini kupata kiharusi. Takwimu zilizochapishwa kwenye jarida la kitabibu la Lancet, linaonyesha upo uwezekano wa … Read More
  • Marufuku kupeana mikono Dar… Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik, amewataka wakazi wa jijini hilo kuchukua hadhari za kiafya ikiwamo kuacha kusalimiana kwa kushikana mikono kutokana na mlipuko wa kipindupindu ambao mpaka sasa umeshawapata wa… Read More

0 comments:

Post a Comment