This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday, 22 April 2013

Kwa nini binadamu hulia?Fahamu sasa..

      Wanawake na wanaume hulia tofauti.. Watafiti wa  nchini Ujerumani walifanya utafiti kuhusu kulia na kubaini kuwa wanawake hulia kati ya mara 30 hadi 63 kwa mwaka na wanaume hulia mara 6 hadi 17 kwa mwaka. Wanaume hulia kwa dakika mbili hadi nne wakati wanawake hulia kwa zaidi ya dakika sita. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Dk Kitila Mkumbo anasema kitendo cha kulia kinatokana na mifumo ya hisia. Anasema...

Sunday, 14 April 2013

Hatari:Aina Mpya ya Kisonono Yasambaa Duniani

ina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono au "gono" ambavyo vinahimili dawa (resistant to drugs) zinazotumika kutibu ugojwa huu imegundulika duniani. Taarifa iliyotolewa na shirika la afya duniani (WHO) hivi karibuni imesema, ugonjwa wa kisonono unaoathiri mamilioni ya watu ulimwenguni umeanza kuwa sugu dhidhi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna hatari ya kutoweza kutibika kabisa. Shirika la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza ufuatlijiaji wa aina hii ya kisonono kutokana na ugonjwa wa kisonono kuwa...

Protini Yagundulika Kusababisha Saratani ya Matiti kwa Wanawake Wanaotumia Vilevi

Kimengenyo (enzyme) ambacho ni protini aina ya CYP2E1 kimegundulika kuwa ndio chanzo kinachochangia wanawake kupata saratani ya matiti kwa wanawake wanaotumia vilevi. Kwa muda mrefu wanasayansi walikuwa wakitafuta uthibitisho wa uhusiano wa kunywa pombe na saratani ya matiti, lakini sasa wameweza kupata uhusiano huo. Protini hii hupatikana kwenye matiti ya wanawake na hivyo kuwaweka kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti kama...

Machungwa, Zabibu Hupunguza Uwezekano wa Kupata Kiharusi?

Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani  umesema ya kwamba kula machungwa na zabibu kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi (Stroke). Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu (Citrus Fruit) pekee kwa  mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla. Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi  Nurse’s...

Friday, 12 April 2013

Upara,sababu ya maradhi ya moyo?....

Wanaume wanaoanza kuwa na upara huenda wakakabiliwa zaidi na tisho la maradhi ya moyo kuliko wenzao waliojaa nywele vichwani. Hii ni kwa mujibu wa watafiti nchini Japan. Utafiti huu uliowahusisha watu elfu 37,000, ulichapisha taarifa kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema kuwa wanaume wanaokuwa na upara kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na maradhi ya moyo. Hata hivyo watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache ikilinganishwa na zile...