Thursday 5 November 2015

Mexico yahalalisha bangi kwa watu 4 tu…..

Jana nilikuwa na story inayohusu bangi, ambapo wapiga kura katika jimbo la Ohio nchini Marekani, wamekataa pendekezo la kuhalalisha matumizi ya bangi katika jimbo hilo.

Sasa leo nakupitishia story inayofanana na hivyo toka huko nchini Mexico, ambako Mahakama kuu nchini humo imetoa amri ya kuliruhusu kundi la wanaharakati nchini humo, kupanda na kusambaza bangi kwa matumizi yao wenyewe.
Hata hivyo kauli hiyo itafanya kazi wa kikundi hicho chenye watu wanne pekee, ambao waliokwenda mahakamani pekee yao kudai haki hiyo.
Wataalamu wanasema kuwa amri hiyo huenda ikafungua milango, itakayoruhusu na kuhalalishwa matumizi ya bangi siku zijazo.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kuwa, amri hiyo inazua mjadala kuhusu njia za kudhibiti matumizi na usambazaji wa madawa ya kulevya.

Wanaharakati wanasema kuwa kushindwa kwa Mexico kuhalalisha matumizi ya bangi, ndiko kulikowawezesha walanguzi wa mihadarati kukolea katika biashara hiyo, na kujivunia mabilioni ya fedha katika faida.

0 comments:

Post a Comment