Tuesday 10 November 2015

Mexico kujadili kuhalisha bangi au la…


Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, amesema kuwa ataanzisha mjadala wa taifa kujadili iwapo wanainchi wanataka baingi iidhinishwe au la.


Rais anasema kuwa watalaamu sasa wanafaa kuja pamoja, ili kujadili hatma ya baadaye ya uidhinishwaji wa bangi nchini Mexico.
Amesema anahisi madaktari, wasomi na pia wanasoshiolojia wanapaswa kutoa mchangao wao katika mjadala huo.
Mexico ni moja wa mataifa yaliyoathirika vibaya na ghasia zinazotokana na magenge ya walanguzi wa madawa ya kulevya.

Vilevile baadhi ya wadau wanashauri kuwa,kuhalalishwa kwa bangi na mihadarati Mexico na Marekani, kutawaondoa walanguzi wa madawa ya kulevya kwenye biashara hiyo, na hivyo kupunguza idadi ya watu wanaouawa katika vita dhidi ya ulanguzi.

0 comments:

Post a Comment