Friday 20 November 2015

New Zealand kupigia kura bendera mpya……

Raia nchini New Zealand wawanapiga kura kuchagua bendera, ambayo huenda ikachukua nafasi ya bendera ya sasa.

Kura hiyo ya maamuzi itapigwa kuanzia leo Novemba 20 hadi Desemba 11, kupitia posta kuamua bendera moja kati ya tano zilizopendekezwa ambayo ni bora zaidi.
Kutafanyika kura nyingine mwaka 2016 kuamua iwapo bendera mpya itakayochaguliwa kwenye kura ya kwanza, inafaa kuchukua nafasi ya bendera ya sasa ambayo huwa na bendera ya Uingereza almaarufu Union Jack.
Waziri Mkuu John Key amesema kuwa,bendera ya sasa haiakisi New Zealand ya sasa.
Aidha anaamini inafanana sana na bendera ya Australia, lakini amekiri kwamba ishara zinaonyesha huenda raia wengi wa New Zealand wakaamua kusalia nayo.
Bendera hizo zimewekwa maeneo mengi kote nchini humo kwa raia kujionea na kufanya uamuzi.

Aidha zinatolewa bure kwa watu na makundi ya kijamii yenye milingoti mitano ya kuzipeperushia.

0 comments:

Post a Comment