Monday, 2 November 2015

Wachina kusubiri hadi Machi kupata watoto wawili………..

Mamlaka kuu inayosimamia upangaji wa uzazi nchini Uchina, imeonya wanandoa nchini humo kwamba sharti waendelee kutii agizo la kuwa na mtoto mmoja kwenye familia hadi sheria ifanyiwe marekebisho mwezi Machi.


Alhamisi ya wiki iliyopita serikali ilitangaza kwamba, ingelegeza sheria na kuwaruhusu wanandoa kuzaa watoto wawili.
Ilisema uamuzi huo ulifanywa kutokana na ongezeko kiwango cha wazee, ukilinganisha na vijana katika jamii na lengo ni kuimarisha uchumi.
Lakini maafisa wamesema sera ya kuwa na mtoto mmoja katika familia, itaendelea kutekelezwa hadi sharia ifanyiwe mabadiliko.
Mnamo Ijumaa afisa mmoja alinukuliwa akisema kwamba wajawazito walio na mimba ya watoto wa pili hawataadhibiwa tena, jambo lililodokeza kwamba sera hiyo tayari ilikuwa imeanza kutekelezwa.
Lakini Jumapili Tume ya Kitaifa ya Afya na Upangaji Uzazi, ilisema maafisa wa serikali wataendelea kutekeleza sheria hizo hadi sheria ifanyiwe marekebisho Machi.

Serikali inakadiria kwamba familia 90 milioni zitapata nafasi ya kuongeza mtoto mwingine, sera ya kuwa na watoto wawili ikianza kutekelezwa.

Related Posts:

  • Ukatili wa kutisha kichanga chaokotwa kimekufa..!! Matukio ya kinyama ya kuwatupa watoto hususani vichanga yameendelea kutokea katika maeneo mbali mbali hapa nchini Tanzania. Jana katika mkoa wa Arusha eneo la  la Relin Themi Njiro, ameokotwa mtoto kichanga ambaye ame… Read More
  • Kesi ya rais wa Kenya yafungwa rasmi Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta . Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia ziliz… Read More
  • Papa Francis atoa ishara za kujiuzulu.!!!!! Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amedokeza kwamba huenda akafuata nyayo za mtangulizi wake Papa Benedict kwa kujiuzulu. Akihojiwa na runinga moja ya nchini Mexico katika sherehe za maadhamisho yake ya p… Read More
  • Mwanamke mwenye 'sura mbaya' atoa filamu.. Mwanamke anayedaiwa kuwa na sura mbaya duniani na mitandao inayomuonea ametoa filamu kuhusu maisha yake. Maisha ya Lizzie Velasquez mwenye umri wa miaka 26 yalibadilika kabisa baada ya kuona kanda ya video katika mtandao… Read More
  • Under 18 Uingereza kufunzwa Somo kuhusu ubakaji.... Wanafunzi kuanzia miaka 11 nchini Uingereza watafundishwa kuhusu tofauti kati ya ubakaji na tendo la ngono ambalo limetekelezwa kutokana na idhini ya wapenzi wawili kama mojawapo ya mipango ya kuwawapa ujuzi kuhusu mais… Read More

0 comments:

Post a Comment