Thursday 26 November 2015

Bila kibali cha daktari huruhusiwi kunywa pombe India………

Licha ya jimbo la Gujarat India kupiga marufuku unywaji utengenezaji na unywaji pombe, takriban watu 60,000 wamepewa idhini ya kunywa pombe.

Takwimu zilizowekwa wazi na idara ya afya inaonesha kuwa watu 60,000 wamepewa idhini na madaktari kunywa pombe katika jimbo hilo ambapo adhabu ya ni kali.
Haijulikani ni ugonjwa upi huo unaotibika na pombe ila inaaminika watu hujilinda kwa idhini hizo za daktari kuepuka hatari ya kushikwa.
Gujarat ndiko alikozaliwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo Mahatma Gandhi.
Jimbo hilo liliharamisha ulevi mwaka wa 1960 kwa heshima wa kiongozi huyo wa taifa.

Ukipatikana ukinywa bila idhini unatozwa faini ya dola 20.

0 comments:

Post a Comment