Mji
mmoja kaskazini mwa Iceland, umekuwa kipeperusha bendera ya taifa nusu mlingoti
kila mkazi wa mji huo anapofariki.
Lakini sasa madiwani wa mji huo
wa Husavik wenye wakazi elfu 2,
wameamua kusitisha utamaduni huo.
Wanasema utamaduni huo sasa
haufai kwa sababu wakazi hawajuani kama ilivyokuwa zamani, na si lazima wakazi
wawe wanamfahamu aliyefariki,hii ni kwa mujibu wa gazeti la Morgun bladid.
Mji wa Husavik
huvutia sana watu wanaofika kutazama nyangumi,lakini diwani mmoja kutoka eneo
hilo anasema kupeperushwa kwa bendera nusu mlingoti huwa kunashangaza watalii.
Uamuzi huo haukupitishwa kwa
kauli moja na kumbukumbu za mkutano huo zilizopakiwa mtandaoni, zinaonyesha
kuna madiwani kadha waliopinga mpango huo.
Mmoja wao Sofia Helgasdottir
aliambia tovuti ya Visir kuwa, utamaduni huo ulianza zamani na wamekuwa nao,
hivyo anafikiri ni utamaduni mzuri sana.
Kuhusu wageni kushangazwa amesema wageni hao ndio
wanaofaa kujifunza tamaduni za wenyeji.
0 comments:
Post a Comment