Tuesday, 10 November 2015

Facebook yaonywa ikome kudukua Ubelgiji…



Mahakama moja nchini Ubelgiji, imeipa Facebook saa 48 kukoma kuwadukua watu ambao hawajajiunga na mtandao huo wa kijamii.

Facebook imesema kuwa itakata rufaa uamuzi huo.
Kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii inadai kuwa, mahakama hiyo imetoa kauli hiyo kwa sababu ya programu ambayo imekuwa ikiitumia nchini humo kwa kipindi cha miaka 5 sasa.
Programmu hiyo inajipachika kwa simu ya mtu aliyeingia kwenye mtandao huo wa Facebook pale hata kama sio hajajiunga na mtandao huo wa kijamii.
Hata hivyo mahakama hiyo Ubelgiji imesema kuwa Facebook haina ruhusa ya kuwadakua watu ambao sio watumizi wa mtandao wake.
Na kama watataka kuwadukua, sharti wapate idhini ya mahakama.
Iwapo Facebook itakataa kutii amri hiyo itatozwa faini ya Euro 250,000 kwa siku.
Programu hiyo aina ya Cookies inapigamsasa mtumiaji wa Facebook ilikubaini kama yeye ama mashine anayoitumia imewahi kutumika kujiunga na mtandao huo wa Facebook.

Msemaji wa Facebook alisema kuwa wamekuwa wakitumia programu hiyo ya Datr kwa zaidi ya miaka 5 na hiyo ndio imekuwa ikisaidia kuhakikisha akaunti za watu bilioni moja u nusu iko salama.

Related Posts:

  • Utafiti: Pilipili huchangia maisha marefu… Kwa miaka mingi sasa binadamu amekuwa akitumia pilipili kuongeza ladha kwenye mlo wake. Kuna wanaovutiwa na ukali wake na vilevile wanaoichukia kutokana na ukali huo. Sasa utafiti umeonyesha si ladha tu ambayo pilipil… Read More
  • Mbwa atumia wiki tatu kujifunza lugha mpya…… Mbwa aliyekuwa akiandamana na mmiliki wake kwenye darasa la kujifundisha lugha, ameshangaza wengi baada ya kuanza kuelewa lugha hiyo baada ya wiki tatu pekee. Neil smith alikuwa akiandamana na mbwa wake mwenye umri wa mi… Read More
  • Nyani wazima kituo cha redio Zimbabwe…… Nyani wasumbufu katika kijiji cha Zvishane mjini Zimbabwe,wamedaiwa kukizama kituo kimoja cha cha redio nchini humo. Mkuu wa kituo cha cha YA FM Munyaradzi Hwengwere, ameliambia gazeti la la serikali Chonicle kwamba, kun… Read More
  • Antenna Show ya radio 5 Tar 30-9-2015 Kama ulimiss kusikia nilichokifanya kwenye Show ya Antenna Tarehe 30-9-2015, basi nimekupachikia hapa twende sawa, show hufanyika siku tano za za wiki yaani Monday to Friday kanzia saa kumi kamili jioni mpaka saa kumi na mbi… Read More
  • Facebook kuanzisha Satelite yao… Kampuni ya Facebook imetangaza kuwa itaanzisha mtandao wa satellite, ili kutoa huduma za internet kwenye maeneo yaliyo mashambani barani Afrika. Kwa ushirikiano na kampuni ya Eutelsat iliyo Ufaransa, Facebook wanatumaini… Read More

0 comments:

Post a Comment