Mashindano
ya kombe la dunia ya mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, yalichochea ongezeko la
idadi ya watoto wa kiume waliozaliwa nchini humo, miezi tisa baada ya
mashindano hayo kuanza.
Hiyo ni kwa mjibu wa taarifa
iliyochapishwa katika jarida la Early Human Development.
Kiwango cha wavulana waliozaliwa
katika kipindi hicho kilikuwa kikubwa mno kati ya miaka 2003 na 2014.
Inasemekana kuwa kutokana na
mchuano huo wa kombe la dunia, wanaume wengi walibaki makwao na hivyo kuchochea
kufufuka kwa ndoa zilizokuwa zimefifia.
Watafiti hao wamesema kuwa watu
walikuwa watulivu zaidi, na kuna uwezekano walijihusisha katika tendo la ndoa
zaidi wakati wa mashindano hayo ya kombe la dunia, hali iliyofanya ongezeko
kubwa ya idadi ya wanawake waliopata ujauzito.
0 comments:
Post a Comment