Wednesday 2 December 2015

Kitabu cha Adolf Hitler kuchapishwa tena…

Kitabu maarufu cha Adolf Hitler kwa jina Mein Kampf kitachapishwa tena kikiwa na maelezo zaidi ya wasomi mwezi ujao, ikiwa ni mara ya kwanza kitabu hicho kuchapishwa tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Taasisi ya Historia ya Kisasa (IfZ) in Munich mjini Munich, imesema itapiga chapa nakala elfu 4.
Mkurugenzi wa IfZ Andreas Wirsching, anasema nakala hizo mpya zina vifungu 3,500 vya maelezo ya ziada, ambayo yatafutilia mbali habari zilisizo za kweli kuhusu kitabu hicho, ambacho kilikuwa manifesto ya kisiasa ya Hitler.
Lakini hatua ya kuchapisha upya kitabu hicho imepingwa na makundi ya Wayahudi, yanayodai kazi za Sanaa za Nazi hazifai kuendelezwa.
Mein Kampf (Mapambano au Mapigano yangu) kilichapishwa mara ya kwanza 1925,miaka minane baada ya Hitler kuindia madarakani.
Baada ya Ujerumani chini ya Wanazi kushindwa kwenye vita 1945,vikosi vya Muungano vilikabidhi jimbo la Bavaria hakimiliki za kitabu hicho.
Viongozi wa eneo hilo walikataa kichapishe tena kuzuia kuenea kwa chuki na uhasama.

Chini ya sheria ya Ujerumani, hakimiliki hudumu miaka 70, hii ikiwa na maana kwamba wachapishaji vitab

0 comments:

Post a Comment