Hali
ya hewa ya El Nino ambayo imekuwa ndiyo kali zaidi katika historia itazidisha
hatari ya njaa na maradhi kwa mamilioni ya watu duniani 2016, mashirika ya
misaada yamesema.
Hali hii ya hewa inatarajiwa
kusababisha ukame baadhi ya maeneo na mafuriko kwingine.
Baadhi ya maeneo yanayotarajiwa
kuathirika sana yako Afrika, huku uhaba wa chakula ukitarajiwa kufikia kilele
Februari.
Maeneo mengine yakiwemo Caribbea,
Amerika ya Kati na Amerika Kusini yataathiriwa katika kipindi cha miezi sita
ijayo.
Hali ya hewa ya El Nino, hutokana
na kuongezeka kwa joto na huathiri hali ya hewa maeneo mengi. Mwaka huu hali
hii imezidi na kuufanya mwaka 2015 kuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika
historia.
Kufikia sasa watu 31 milioni
wanakabiliwa na uhaba wa chakula Afrika, theluthi moja kati ya hawa wakiwa
Ethiopia.
Inakadiriwa kwamba watu 10.2
milioni watahitaji chakua cha msaada mwaka 2016.
Mashirika ya misaada kama vile
Oxfam yameelezea wasiwasi kwamba athari za El Nino zitazidisha makali ya mizozo
ya sasa kama vile vita Syria, Sudan Kusini na Yemen.
Hali ya hewa ya El Nino
inatarajiwa kumalizika katikati mwa mwaka ujao.
Kuna wasiwasi kwamba hali hii
huenda ikafuatwa na hali ya La Nina ambayo katika maeneo mengi husababisha
ukame.
Hali kama hii ilifuata mvua kubwa
1997/98.
El Nino hutokana na kuongezeka
kwa joto baharini nayo hali ya La Nina husababishwa na kushuka kwa viwango vya
joto baharini.
0 comments:
Post a Comment