Tuesday 29 December 2015

Mbwa aliyeuawa kupewa nishani ya ushujaa...!!

Mbwa wa polisi aliyeuawa wakati wa msako baada ya mashambulio ya Paris, atatunukiwa nishani kuu ya ushujaa.

Diesel mbwa aina ya Belgian Shepherd mwenye umri wa miaka saba, alifariki wakati wa operesheni ya kumsaka mshukiwa mkuu wa mashambulio hayo.
Mbwa huyo atatunukiwa nishani kwa jina Dickin Medal, ambayo hutolewa na shirika la kuwatunza wanyama la PDSA.

Hadhi ya nishani hiyo ni sawa na nishani ya Msalaba wa Victoria,inayopewa watu mashujaa vitani.

0 comments:

Post a Comment