Wednesday 2 December 2015

Unawajua wanaongoza kwa ufisadi zaidi Afrika……?

Wafanyibiashara wakubwa Africa, wametakwa kuwa miongoni mwa watu wafisadi zaidi sawa na maafisa wa polisi Barani Afrika.

Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa na shirika la kuchunguza ufisadi duniani Transparency International.
Hii ni mara ya kwanza wafanyibiashara wametajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani Africa.
Shirika hili limeongeza kwamba utumizi mbaya wa mamlaka, unasababisha ongezeko la umasikini, na kuwanyima raia mahitaji muhimu.
Watu wengi ambao ni masikini wamejikuta mara kadhaa wakilazimika kulipa hongo, ikilinganishwa na matajiri inasema sehemu ya taarifa hiyo ya Transparency International.
Nchi ya Liberia imetajwa kama nchi inayoongoza kwa visa vya ufisadi Afrika,inafuatwa na Cameroon, Nigeria na Sierra leone.
Afrika mashariki Uganda inaongoza kwa visa vya ufisadi, ikifuatwa na Kenya.
Kusini mwa Afrika Zimbabwe na Zambia zinaongoza katika nchi zenye visa vingi vya ufisadi.

Botswana, Mauritius na Cape Verde, ndiyo mataifa pekee ya Afrika ambapo visa vya ufisadi ni vya chini zaidi ikiwa ni asili mia mbili pekee.

0 comments:

Post a Comment