Monday 7 December 2015

Je kuna nini kilomita 5 chini ya bahari…?

Wanasayansi wa Uingereza wanapanga kuchimba chini kabisa ya ardhi katika bahari Hindi.

Lengo ni kufika chini zaidi ya tabaka za juu za ardhi, kwa mara ya kwanza.
Wanataka kuchunguza udogo kutoka ndani ya ardhi, na kuthibitisha yale yanayojulikana kuhusu umbo la ardhi.
Shughuli hizo zitachunguza iwapo kuna viumbe hai ndani zaidi ya ardhi kushinda vile vinavyojulikana.
Zimefanywa juhudi mara kadha kuchimba ndani ya zaidi ya tabaka za juu za ardhi, lakini hazikufanikiwa.

Hata hivyo wataaalamu wa wanaohusika na maswala ya sayansi, wanasema kuchimba ardhi kina cha kilomita 5 chini ya bahari ni kazi kubwa, na hadi sasa teknolojia imeshindwa.

0 comments:

Post a Comment