Friday 11 December 2015

Mwanajeshi ashambuliwa na duma akipiga picha…

Jeshi la wanahewa la Afrika Kusini limesema kuwa,duma wawili ambao hufugwa kwenye kambi ya jeshi hilo ili kufukuza wanyama wengine kwenye njia ambayo hutumiwa na ndege kupaa, wamemshambulia afisa wa jeshi.

Msemaji wa jeshi hilo Marthie Visser amesema kupitia taarifa kwamba, duma hao waliingia eneo ambalo ndege huegeshwa katika eneo la Makhado.
Mwanajeshi aliyekuwa kwenye zamu aliwaona na kujaribu kuwapiga picha, na hapo ndipo wakamshambulia.
Mwanajeshi huyo hakujeruhiwa vibaya na ameruhusiwa kutoka hospitalini,baada ya kupatiwa matibabau.
Hata hivyo uongozi umesema wanyama hao hawatafukuzwa katika kambi hiyo.

Bi Visser amesema kambi hiyo iliyo kaskazini mwa Afrika Kusini, imezingirwa na mbuga za wanyama na duma hao husaidia kudhibiti ongezeko la wanyama mwitu.

0 comments:

Post a Comment