Friday, 4 December 2015

Aliyewaambukiza watu 200 HIV afungwa miaka 25...!

Daktari aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini Cambodia amehukumiwa jela.

Daktari huyo bandia alipatikana na hatia ya kuwaambukiza takriban watu 200 virusi vya ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa yake.
Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia.
Yem Chrin alikuwa akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji cha Roka bila ya kujua alikuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi.
Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji, lakini upande wa mashtaka ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.
Kesi hiyo imefichua uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa raia kupata huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.

Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini, huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.

Related Posts:

  • Usikose nakala yako ya gazeti la TABIBU kesho alhamisi likiwa limesheheni habari kemkem za afya. Ni kwa bei ya sh. 500/= tu. TABIBU michezo wiki hii.!! … Read More
  • Je wajua siri ya Mamba usingizini….? Wataalamu wa masuala ya wanyama wamegundua kwamba, mamba ana uwezo wa kulala huku jicho lake moja likiwa wazi. Utafiti huo ambao umewaacha wengi wakishangaa, kwani picha nyingi duniani huonyesha kuwa mamba hulala fofofo,… Read More
  • Je Aspirin inazuia kurejea kwa Saratani…..? Utafiti mkubwa na wa kwanza kubaini iwapo umezaji wa tembe za Aspirin kila siku unapunguza kwa kiwango kikubwa athari ya kurejea kwa saratani umeanza nchini Uingereza. Jaribio hilo litahusisha watu 11,000 wanaotibiwa a… Read More
  • Filamu mpya ya Stars Wars yavunja rekodi… Filamu mpya ya Star Wars: The Force Awakens imevunja rekodi Uingereza kwa kuuza tikezi nyingi zaidi siku ya kwanza ya kuuzwa kwa tiketi. Tiketi hizo za mapema zilianza kuuzwa Jumanne, huku filamu hiyo ikitarajiwa kuto… Read More
  • Usikose kusoma nakala yako ya gazeti la TABIBU leo alhamisi liko mitaani kwa bei ya sh. 500/= tu. Utapata kujua undani wa tiba za asili na kisasa kuusu magonjwa mbalimbali. "TABIBU NI DAKTARI WAKO WA NYUMBANI"   … Read More

0 comments:

Post a Comment