Monday, 28 December 2015

Mlinzi wa Osama bin Laden afariki dunia…

Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Vyanzo vya habari vya kitabibu vimeiambia BBC kwamba Nasser al Bahri,ambaye pia alikuwa akijulikana kama Abu Jandal alifariki siku ya Jumamosi, katika Hospitali iliyoko kwenye mji wa Mukalla kusini mwa Yemen.

Alirudi nchini humo mwishoni mwa mwaka 2008 baada ya kuachiliwa kutoka katika kizuizi, alichowekewa na Marekani huko Guantanamo.

Al Bahri alijulikana kuhusika na mashambulizi yaliyofanywa na mtandao wa kigaidi katika miaka ya 90, katika nchi za Afghanistan, Somalia na Bosnia.

Related Posts:

  • MWANAMKE MTUMWA KUWEKWA KWENYE DOLA MAREKANI… Picha ya mtumwa mmoja aliyekata nyororo na kisha kusaidia mamia ya wenzake kutoroka utumwa, sasa itatumika katika noti mpya ya dola 20 nchini Marekani. Bi Harriet Tubman atakuwa Mwafrika Mmarekani wa kwanza, kuingizwa k… Read More
  • MSOMI AVUA NGUO KWA KUFUNGIWA OFISI… Hatua ya mwanamke mmoja msomi ya kuvua nguo nchini Uganda, imezua mjadala mkali nchini humo. Baada ya kukerwa na hatua ya kufungiwa nje ya ofisi yake na usimamizi wa chuo kikuu cha Makerere, Stella Nyanzi alivua nguo zo… Read More
  • WANANE MBARONI KWA KUNYWA POMBE MCHANA… Wilaya ya Sengerema imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais, baada ya kukamata watu wanane waliokutwa wakinywa pombe saa za kazi. Amri ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa watu hao ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilay… Read More
  • CANADA KUHALALISHA MATUMIZI YA BANGI..!! Serikali ya Canada itabuni sheria mpya mwaka ujao, ambazo zitahalalisha uuzaji wa bangi. Iwapo sheria hiyo itaidhinishwa italiorodhesha taifa la Canada, miongoni mwa mataifa yenye uchumi mkubwa magharibi kukubali matumi… Read More
  • MALKIA ELIZABETH ATIMIZA MIAKA 90… Siku ya leo tarehe 21-4-2016 Malkia Elizabeth ametimiza miaka tisini ya kuzaliwa. Malkia atasheherekea siku hii kwa kukutana na wananchi wake katika matembezi atayafanya huko Windsor. Malkia Elizabeth ametawala kwa mu… Read More

0 comments:

Post a Comment