Wednesday 9 December 2015

Malaysia yatafuta mmiliki wa ndege zilizoachwa uwanjani…

Serikali ya Malaysia imeweka tangazo magazetini,ikitafuta mmiliki wa ndege tatu aina ya Boeing 747 ambazo zimeachwa katika uwanja wa ndege Kuala Lumpur.

Tangazo hilo lililotolewa na mamlaka ya viwanja vya ndege,limeonya mmiliki wa ndege hizo kwamba akikosa kwenda kuzidai katika kipindi cha siku 14 zijazo, basi watakuwa na haki ya kuziuza au kuzitumia kwa namba nyingine.
Mamlaka hiyo imesema ndege hizo pia hazijalipiwa ada ya kutua na ada ya maegesho.
Amesema kwa miongo kadha sasa kuna ndege ambazo zimekuwa zikiachwa uwanjani lakini sana huwa ni ndege ndogo.
Moja iliyoachwa miaka ya 1990 iliuzwa na baadaye ikaanza kutumiwa kama mgahawa katika kitongoji kimoja cha mji wa Kuala Lumpur.

Maafisa wanasema malipo yasipopokelewa kufikia Desemba 21,ndege hizo zitapigwa mnada au ziuzwe zitumiwe kama vyama vikukuu kulipa gharama.

0 comments:

Post a Comment