This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Friday, 6 March 2015

Tamko la Facebook lamtia mashakani

Raia mmoja wa Marekani anayefanya kazi katika mataifa ya milki za kiarabu UAE, amekamatwa kwa matamshi aliyochapisha katika mtandao wake wa facebook na sasa anakabiliwa na hukumu ya kufungwa jela. Ryan Pate ambaye ni fundi wa ndege,alikuwa katika likizo ya kujiuguza nyumbani kwake katika jimbo la Florida nchini Marekani wakati alipomkosoa mwajiri wake. Aliita kampuni hiyo kama yenye ''wasaliti na kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya watu wa mataifa ya milki hiyo. Wakati alipokuwa akirudi alikamatwa kwa kukiuka sheria kali za taifa hilo kuhusu matamshi ya kashfa. Iwapo atapatikana na hatia huenda akahudumia kifungo cha hadi miaka mitano jela.

Monday, 22 April 2013

Kwa nini binadamu hulia?Fahamu sasa..

 

 

 

Wanawake na wanaume hulia tofauti..

Watafiti wa  nchini Ujerumani walifanya utafiti kuhusu kulia na kubaini kuwa wanawake hulia kati ya mara 30 hadi 63 kwa mwaka na wanaume hulia mara 6 hadi 17 kwa mwaka.


Wanaume hulia kwa dakika mbili hadi nne wakati wanawake hulia kwa zaidi ya dakika sita.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Dk Kitila Mkumbo anasema kitendo cha kulia kinatokana na mifumo ya hisia.
Anasema binadamu huweza kulia kutokana na hasira, maumivu au furaha.
Zipo aina tatu za machozi
Binadamu yeyote ana mirija ya machozi ambayo hutumika kulowanisha na kulinda macho yasiathiriwe na vumbi na vitu vingine.
Mirija hiyo ipo chini ya kope za juu na huzalisha maji yenye chumvichumvi ambayo ndiyo machozi-hayo  husambazwa katika jicho- kila  binadamu anapopepesa.
Wanasayansi wanasema, zipo aina tatu za machozi ambazo huzalishwa na macho ya binadamu.
Yapo machozi yajulikanayo kama ‘Basal’ au Basali. Machozi haya yana kazi kubwa ya kulinda jicho na kulipa unyevu.
Machozi mengine ni ya ‘Reflex’ haya yana kazi kubwa ya kutoa tahadhari kwa jicho pale linapoumia. Kwa mfano mtu akikata kitunguu au mdudu akiingia jichoni.
Machozi ya hisia au  ‘Pysch’ haya hutiririka pale ambapo binadamu hupatwa na uchungu, maumivu, msongo wa mawazo au furaha.
Tafiti zinaonyesha kuwa machozi ya hisia yana kiwango cha manganizi, chembechembe ambazo huathiri tabia au roho ya binadamu.
Machozi hayo ya hisia pia yana vichocheo vya prolactini ambavyo husimamia uzalishwaji wa maziwa.
Machozi yanayozalishwa kwa hisia yana mchanganyiko wa kemikali tofauti na aina nyingine za machozi.


Hivyo basi, binadamu anapolia, hutoa manganizi, potashiam na prolactini.
Chembechembe hizo zinatajwa kupunguza mshtuko au huzuni kwa  kuweka uwiano wa msongo wa mawazo katika mwili.

Sunday, 14 April 2013

Hatari:Aina Mpya ya Kisonono Yasambaa Duniani

ina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono au "gono" ambavyo vinahimili dawa (resistant to drugs) zinazotumika kutibu ugojwa huu imegundulika duniani. Taarifa iliyotolewa na shirika la afya duniani (WHO) hivi karibuni imesema, ugonjwa wa kisonono unaoathiri mamilioni ya watu ulimwenguni umeanza kuwa sugu dhidhi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna hatari ya kutoweza kutibika kabisa.
Shirika la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza ufuatlijiaji wa aina hii ya kisonono kutokana na ugonjwa wa kisonono kuwa na athari nyingi kama mcharuko (inflammation), ugumba, matatizo wakati wa ujauzito na hata vifo vya kina mama wajawazito.
“Aina hii mpya ya vimelea vya kisonono vinaonyesha usugu dhidhi ya dawa zote za antibiotiki tunazotumia dhidhi yake ikiwemo dawa za jamii ya cephalosporins ambazo ni dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa wa kisonono, “ alisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan, mmoja wa wanasayansi wa shirika la afya duniani katika kitengo cha magonjwa ya zinaa.
Miaka michache ijayo, aina hii mpya ya kisonono itakuwa sugu dhidhi ya dawa zote ambazo tunazo saizi “aliendelea kusema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan wakati wa mahojiano na shirika la habari la The Associated Press kabla WHO haijatangaza rasmi hatua na mwongozo mpya wa kukabiliana na tishio la aina hii mpya ya kisonono.
Inakisiwa watu milioni 106 ulimwenguni kote huathiriwa na ugonjwa wa kisonono kila mwaka.Ugonjwa wa kisonono pia huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Virusi vya Ukimwi (VVU).
“Ugonjwa sugu wa kisonono sio tatizo la bara la Ulaya au Afrika pekee bali ni tatizo la dunia nzima kwa sasa,’” alinukuliwa akisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan.
Kwa mara ya kwanza, vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidhi ya dawa aina ya cephalosporins  viliripotiwa katika nchi ya Japan, ikifuatiwa na Uingereza, Hongkong na Norway.
Wanasayansi wanaamini matumizi mabaya ya dawa aina ya antibiotiki pamoja na uwezo wa vimelea vya ugonjwa wa kisonono kubadilika na kuzoea mazingira mapya ndio chanzo kikuu cha kutokea kwa ugonjwa sugu wa kisonono na hivyo muda si mrefu ugonjwa huu utakuwa janga kubwa dunia nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa. Kuna uwezekano wa vimelea hivi sugu vya kisonono vinasambaa kwa sasa duniani bila kuweza kugundulika kutokana na nchi nyingi kutokuwa na ufuatiliaji na utunzaji kumbukumbu  mzuri wa wagonjwa wake.
Shirika la afya duniani limesema nchi zinatakiwa kuongeza ufuatiliaji wa wagonjwa wake pamoja na kudhibiti matumizi holela ya dawa za antibiotiki mpaka pale taarifa kamili za ugonjwa huu zitakapojulikana.
“Elimu ya masuala ya kujamiana pamoja na matumizi sahihi ya mipira ya kondomu inahitajika ili kutokomeza kabisa ugonjwa huu sugu wa kisonono. Hatuwezi kuutokomeza kabisa ugonjwa huu bali tunaweza kuzuia usambaaji wake,”alisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan.

Protini Yagundulika Kusababisha Saratani ya Matiti kwa Wanawake Wanaotumia Vilevi

Kimengenyo (enzyme) ambacho ni protini aina ya CYP2E1 kimegundulika kuwa ndio chanzo kinachochangia wanawake kupata saratani ya matiti kwa wanawake wanaotumia vilevi. Kwa muda mrefu wanasayansi walikuwa wakitafuta uthibitisho wa uhusiano wa kunywa pombe na saratani ya matiti, lakini sasa wameweza kupata uhusiano huo. Protini hii hupatikana kwenye matiti ya wanawake na hivyo kuwaweka kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti kama watakuwa wanakunywa sana vilevi kama pombe, whiskey, wine na nk.
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Autonomous University of the State of Morelos cha nchini Mexico, umeonyesha ya kwamba protini hiyo ya aina ya CYP2E1 inauwezo wa kukivunja vunja kilewesho (ethanol) na kusababisha kutolewa kwa kemikali hatari zinazojulikana kama free radicals.
Watafiti hao wamesema ugunduzi wao utasaidia katika kuvumbua kipimo kitakachosaidia kujua ni wanawake gani walio na protini hii ya CYP2E1 na hivyo kuwasaidia kujikinga dhidhi ya saratani ya matiti.
Kemikali hizi hatari uhusishwa na kutokea kwa baadhi ya magonjwa kama saratani mbalimbali, ugonjwa wa kisukari, uharibifu wa mishipa ya damu aina ya ateri (arteries), kuchangia mtu kuzeeka na nk.
Swali kuu walilojiuliza watafiti wakati wa utafiti huo ni , Je kuwa na protini hii ya CYP2E1 kwa wingi huchangia mwanamke kupata ethanol-induced toxicity na hivyo kumhatarisha kupata saratani ya matiti?
Matokeo yetu yalionyesha ya kwamba seli za kutoka katika matiti ya mwanamke (mammary cells) zilizowekwa kilewesho cha aina ya ethanol, hutoa kemikali hatari kwa wingi, husababisha kuwepo kwa oxidative stress, huharakisha ufanyaji kazi wa seli na hivyo kuongeza kiwango cha ukuaji wa seli hizi kwa wingi na kusababisha saratani ya matiti” alisema Profesa Maria de Lourdes Rodriguez-Fragoso, kutoka chuo kikuu cha The Autonomous University of the State of Morelos cha nchini Mexico.
“Kama wewe ni mwanamke ambaye una kiwango kikubwa cha protini hii ya CYP2E1 katika matiti yako na unakunywa pombe basi utakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti ikilinganishwa na mwanamke ambaye ana kiwango kidogo cha protini hii katika matiti yake.” Aliendelea kusema Profesa Maria de Lourdes Rodriguez-Fragoso.
Uchunguzi uliofanywa kutoka kwenye tishu za matiti ya wanawake wenye afya njema ambao wamefanyiwa upasuaji wa kukuza matiti yao umeonyesha viwango tofauti vya protini hii katika wanawake hawa.
“Hii inamaanisha ya kwamba wanawake wanatafautiana kwa umengenywaji wa pombe na hivyo inabidi kila mwanamke kuchukua hatua tofauti katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti” Alisema tena Profesa Maria de Lourdes Rodriguez-Fragoso.
Protini hii ya aina ya CYP2E1 hupatikana katika seli za matiti ya mwanamke zinazojulikana kama mammary epithelial cells ambapo pia ndio chanzo cha seli/chembechembe nyingi za saratani ya matiti na kusababisha watafiti hao kuanza kushuku uhusiano wake na saratani ya matiti.
Ili kuthibitisha shauku yao kwamba protini hii husababisha saratani ya matiti, watafiti hao walichukua tishu za matiti zilizo na viwango tofauti vya CYP2E1 na kuziweka kwenye pombe. Matokeo yalionyesha ya kwamba seli zenye kiwango kidogo cha protini aina ya CYP2E1 hazikuathiriwa sana ikilinganishwa na seli ambazo zilikuwa na kiwango kikubwa cha protini hiyo.
Utafiti huu ni ushindi mkubwa katika vita dhidhi ya saratani ya matiti kwani utasaidia kupunguza kiwango cha saratani hii kwa wanawake

Machungwa, Zabibu Hupunguza Uwezekano wa Kupata Kiharusi?

Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani  umesema ya kwamba kula machungwa na zabibu kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi (Stroke).
Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu (Citrus Fruit) pekee kwa  mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla.
Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi  Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida hizo za machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume.
 
Timu ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo Kikuu cha  East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina ya flavonoids ambayo ni jamii ya antioxidant (kemikali zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana katika matunda, mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu.
 
Utafiti huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 ambao walikuwa wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha kula matunda na mboga za majani kwa kila kipindi cha  miaka 4. Timu hiyo ya utafiti iliangalia uhusiano wa aina sita ya flavonoids - flavanones, anthocyanins, flavan-3-ols, flavonoid polymers, flavonols na flavones na hatari ya aina mbalimbali za kiharusi kama Ischaemic, Hemorrhagic na Total Stroke. Ilionekna wanawake waliokula kiwango kikubwa cha flavanones kwenye matunda chachu walikuwa na asilimia 19 ya uwezekano wa kupunguza kiharusi kulinganisha na wanawake ambao walikula kiwango kidogo cha matunda hayo.
 
Kiwango kikubwa cha flavanones kilikuwa 45mg kwa siku kulinganisha na kiwango kidogo cha  25mg kwa siku. Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la Medical Journal Stroke umesema flavanones hupatikana kwa asilimia 82 kwenye machungwa na juisi ya machungwa na hupatikana kwa asilimia 14 kwenye zabibu na juisi ya zabibu.
 
Hata hivyo watafiti hao wamesema kwa wale wenye kusudio la kuongeza kiwango kikubwa cha flavanones itawalazimu kula tunda la chungwa kwa wingi na si juisi za machungwa zinazotengenezwa kiwandani kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachopatikana katika juisi hizo za viwandani.
 
Professa Aedin Cassidy wa masuala ya lishe bora (nutrition) na ambaye alikuwa kiongozi wa utafiti huo amesema “kula kwa wingi kwa matunda, mboga za majani, na hasa Vitamin C uhusishwa na kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi”. Flavanones hutoa kinga dhidhi ya kiharusi kutokana na kuongeza ufanisi wa mishipa ya damu kwenye ubongo na kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi mwilini (Anti-inflammatory effect).
 
Utafiti uliofanyika hapo awali ulionyesha ya kwamba ulaji wa matunda chachu na juisi yake na si matunda ya aina nyingine yoyote hupunguza uwezekano wa kupata  kiharusi aina ya Ischaemic Stroke na kuvuja damu kwenye ubongo (Intracerebral Haemorrhage).
 
 
Utafiti mwingine uliofanyika kipindi cha nyuma ulionyesha hakuna uhusiano wowote wa matunda ya njano na machungwa katika kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi lakini ulionyesha ya kwamba kuna uhusiano wa zabibu na mapeasi wa kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.
 
Katika utafiti mwingine uliofanyika nchini Sweden umeonyesha ya kwamba wanawake ambao walikula  kiwango kikubwa cha antioxidant karibia asilimia 50 kutoka kwenye matunda na mboga za majani, ni wachache tu kati yao waliopata kiharusi ikilinganishwa na wanawake ambao walikuwa na kiwango kidogo cha antioxidant.
 
Matokeo ya utafiti huu yasiwafanye watu kuacha kula matunda ya aina nyingine pamoja na mboga za majani kwani nayo yana faida kubwa katika mwili wa binadamu.
 
Kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi inawezekana kama mtu atakula lishe bora iliyo na virutubisho vyote muhimu, kula matunda na mboga za majani kwa wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza kiwango cha ulaji chumvi (kwani watu wenye asili ya Kiafrika wana kiashiria cha asili kinachojulikana kama salt retention gene ambacho hufanya kiwango kidogo cha matumizi ya chumvi mwilini kuonekana kama kiwango kikubwa na hivyo kuongeza hatari ya kupata kiharusi),kupunguza uzito (kuwa kwenye uzito unaotakikana kiafya  kulingana na umri na urefu wako), kupunguza kiwango cha matumizi ya mafuta katika chakula, kulala masaa ya  kutosha na kupunguza msongo wa mawazo. 


Friday, 12 April 2013

Upara,sababu ya maradhi ya moyo?....



Wanaume wanaoanza kuwa na upara huenda wakakabiliwa zaidi na tisho la maradhi ya moyo kuliko wenzao waliojaa nywele vichwani.
Hii ni kwa mujibu wa watafiti nchini Japan.
Utafiti huu uliowahusisha watu elfu 37,000, ulichapisha taarifa kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema kuwa wanaume wanaokuwa na upara kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na maradhi ya moyo.

Hata hivyo watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache ikilinganishwa na zile za uvutaji sigara na unene kupita kiasi.

Shirika linalojikita katika maswala ya maradhi ya moyo nchini Uingereza, limesema kuwa wanaume wanapaswa kujichunga wasinenepe kupita kiasi kuliko kuchunga nywele zao.

Kuanza kukuwa na kipara ni kawaida ya maisha kwa wanaume .

Wengi kuanza kukuwa na upara wanapokuwa miaka 50 na asilimia 80 ya wanaume hao, hupoteza nywele wanapokuwa na umri wa miaka 70.

Watafiti katika chuo kikuu cha Tokyo, walidurusu utafiti wa miaka mingi iliyopita, kuchunguza uhusiano uliopo kati ya kuwa na upara na maradhi ya moyo.

Walionyesha kuwa nywele ambazo zilianza kutoweka, zina uhusiano na maradhi ya moyo.

Hii ilikuwa baada ya kuzingatia maswala kama umri, na historia ya familia.

Daktari Tomohide Yamada wa chuo kikuu cha Tokyo,amesema kuwa walipata uhusiano mkubwa kati ya upara na tisho la kupata maradhi ya moyo.

Amesema kuwa wanaume wenye umri mdogo wanaopata upara wanapaswa kuanza kuzingatia afya njema ili kujikinga kutokana na maradhi ya moyo

Aidha amesema hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza kuwa wanaume wenye upara wafanyiwe uchunguzi wa maradhi ya moyo.

Maradhi ya moyo ndio moja ya sababu kuu za vifo nchini Uingereza.

Mmoja kati yawanawake wanane kufariki kutokana na maradhi ya moyo.

Husababishwa na mishipa ya damu ambayo husukuma damu kwa moyo pale inapoziba.

Mmoja wa madaktari wakuu Uingereza amesema kuwa ingawa utafiti huu unaibua hisia, wanaume wenye upara hawapaswi kuwa na hofu.

Wednesday, 27 February 2013

Hivi ni vivutio vya Tanzania vilivyoingia katika maajabu saba ya asili Afrika. Serengeti Migration, Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro crater.

Ni Katika kile kinyang'anyiro cha kupata vivutio asilia saba vyenye maajabu toka barani Afrika. Kinyang'anyiro ambacho kilirindima mwaka jana 2012 kwa wadau kupigia kura vivutio 11 vilivyokuwa vikishindanishwa. Mlima Kilimanjaro,Wanyama wanaohama wa Serengeti na Ngorongoro crater ndio yalikuwa maajabu toka Tanzania ambayo yalikuwa yameteuliwa kupigiwa kura,kwa kifupi vivutio vyote vitatu toka Tanzania vimeweza kufanya vyema. Taarifa ya vivutio vitatu kutoka Tanzania kuingia kwenye orodha ya vivutio 7 vya ajabu barani Afrika iliwekwa wazi mjini Arusha,ambako kulikuwa na sherehe rasmi ya kuvitaja vivutio vilivyoingia kwenye orodha hii baada ya zoezi la kupiga kura kusitishwa mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka 2012. Katika hafla hiyo,Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio alikuwa mgeni rasmi. Matokeo hayo yalitangazwa na Dk,Phillip Imler ambaye ni rais wa taasisi ya Seven Natural wonders of the world. Vivutio vingine viliweza kuingia kwenye orodha hii ni Okavango Delta, Red Sea Reef, Jangwa la Sahara na Mto Nile. Tanzania ndio nchi pekee iliyoweza kuingiza vivutio 3 kwenye orodha hii kwa mwaka 2012. Kiwale11 Bloga inatoa pongezi kwa wote waliotikia wito na kupiga kura na kuiwezesha nchi yetu kutoka kifua mbele kwa kuingiza vivutio 3 kwenye orodha hii.

Mazoezi makali yanaongezea umri?..

Wewe ni mkimbiaji au muinua vyuma? Wakimbia katika mbio za masafa marefu au katika mashindano ya michezo mitatu tofauti - triathlon? Ni mazoezi yapi ambayo unaweza kufanya ikiwa unataka kujiongezea umri? Je, ni vyema zaidi kufanya mazoezi mafupi na makali, au marefu zaidi lakini ya taratibu? Kwa mujibu wa Daktari Jamie Timmons, Profesa wa masomo ya bayologia ya uzee katika Chuo Kikuu cha Birmingham, dakika tatu za mazoezi makali kila juma kwa majuma manne kunaweza kukaboresha, kwa kiwango kikubwa, afya ya mtu. Mazoezi haya makali yanaweza kusaidia moyo na mapafu yako kusambaza hewa mwilini vyema zaidi. Pia yanaboresha ifanyavyokazi insulini, ambayo inaondoa sukari mwilini na kudhibiti mafuta. Nao utafiti wa Daktari Stuart Gray wa Chuo Kikuu cha Aberdeen unadhihirisha kwamba mazoezi makali na mafupi, kama kukimbia kwa kasi kwa masafa mafupi, au kuendesha baiskeli kwa sekunde 30 tu, kunaufanya mwili uondoe mafuta kutoka kwenye damu haraka zaidi kuliko kufanya mazoezi ya wastani, kama kutembea harakaharaka. Kuondolewa kwa mafuta kutoka kwenye damu ni muhimu kwa vile kunapunguza uwezekano wa kukumbwa na tukio la mshtuko wa moyo.

WABUNGE WAZICHAPA WAKATI WA MDAHALO KWENYE TV.SHOW

a href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhvUE-3IdrVzVDdRAkVbf9UX_oBv3ikVHMaFcJI1Y3xPsFr_S-9GkT88Na1XAkSmD_3ueR2QJbG30bDAu7srtfgqdHUhYVAVmDz59yOUyI-nEgLEKJGZgtFUO6Q-_ipPrX4GghyROySGXX3/s1600/wabunge.jpg" imageanchor="1" > Wabunge wawili wapigana makonde wakati wa kipindi cha mdahalo kwene runinga ya kitaifa huku Georgia. Huko Lebanon wabunge wengine wawili pia warushiana glasi za maji na baadae kupigana ngumi vilevile wakati wa mdahalo kwenye Televisheni. Hii ni baada ya wabunge hao kuhitalafiana kuhusu vita vinavyoendelea nchini Syria baina ya waasi na serikali ya Rais Basher al Assad.

Monday, 17 December 2012

Fahamu Siri ya herufi ya mwanzo ya Jina lako...

Je Unajua Siri ya herufi ya mwanzo ya jina lako?. Soma hapa utaweza kuelewa Tabia zako au tabia za rafiki au mpenzi wako. >HERUFI A >Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira. Herufi A inawakilisha Nyota ya Punda. >HERUFI B >Mwenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake. Herufi B inawakilisha Nyota ya Ngombe, >HERUFI C >Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano Herufi C inawakilisha Nyota ya Mapacha, >HERUFI D >Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo. Herufi C inawakilisha Nyota ya Kaa, >HERUFI E >Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu. Herufi E inawakilisha Nyota ya Simba, > >HERUFI F >Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi. Herufi F inawakilisha Nyota ya Mashuke, >HERUFI G >Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu. Herufi G inawakilisha Nyota ya Mizani, >HERUFI H >Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi. Herufi H inawakilisha Nyota ya Nge, >HERUFI I >Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka. Herufi I inawakilisha Nyota ya Mshale, >HERUFI J >Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo. Herufi J inawakilisha Nyota ya Mbuzi, >HERUFI K >Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha. Herufi K inawakilisha Nyota ya Ndoo, >HERUFI L >Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara. Herufi L inawakilisha Nyota ya Samaki, >HERUFI M >Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi M inawakilisha Nyota ya Punda >HERUFI N >Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana. Herufi N inawakilisha Nyota ya Ngombe > >HERUFI O >Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia. Herufi O inawakilisha Nyota ya Mapacha >HERUFI P >Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi P inawakilisha Nyota ya Kaa >HERUFI Q >Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana. Herufi Q inawakilisha Nyota ya Simba >HERUFI R >Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani. Herufi R inawakilisha Nyota ya Mashuke >HERUFI S >Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi S inawakilisha Nyota ya Mizani >HERUFI T >Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika. Herufi S inawakilisha Nyota ya Nge >HERUFI U >Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mshale. >HERUFI V >Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mbuzi. >HERUFI W >Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari. Herufi W inawakilisha Nyota ya Ndoo. >HERUFI X >Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota ya Samaki. >HERUFI Y (YASINTA) >Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha. Herufi Y inawakilisha Nyota ya Punda >HERUFI Z >Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo. Herufi Z inawakilisha Nyota ya Ngombe.

Wednesday, 12 December 2012

UNAJUA KUWA SHULE YA KWANZA TANZANIA ILIJENGWA MUHEZA TANGA?

HAYA NI BAADHI YA MAJENGO YALIYOJENGWA KATIKA SHULE HIYO BAADAE.... MWAKA 1848 Mmishenari wa Kijerumani Dk Johan Ludwig Krapf,alitembelea kijiji cha Magila kilichopo Muheza mkoani Tanga akiwa katika safari zake za Afrika Mashariki. Magila kuna mlima ulio katika safu za milima ya Usambara ukipakana na mlima wa Magoroto ambao ndio chanzo cha maji ya mto Mkurumuzi unaoelekea Muheza. Historia inaonyesha eneo la mlima Magila wenye miamba na mawe mengi, zamani kabla ya kuja wageni lilitumika kuwatenga wagonjwa wa ukoma na magonjwa mengine yasiyotibika, kwa lengo la kuwazuia wasiwaambukize wengine. Dk Krapf alipofika na kuwaona wagonjwa hao waliokuwa wakiishi kwa madhila makubwa, alichonga msalaba katika mti wa mkuyu kwa imani kuwa Mwenyezi Mungu angewaponya wagonjwa hao. Eneo hilo ndilo lililokuja kujengwa shule ya kwanza na Waingereza mwaka 1886. Alama ya msalaba huo ipo hadi na sasa na ndipo ilipo Shule ya Sekondari Hegongo. Hadi leo mahali hapo panaitwa Magila Msalabani. Kwa sasa Magila ni kata yenye vijiji vya vya Magila, Mikwamba, Misongeni na Mafleta. Mkaazi wa eneo hilo Luteni Kanali mstaafu John Mhina amekamilisha kuandika kitabu kuhusu historia ya Magila Msalabani,kinachoeleza historia ya kijiji hicho na ujio wa wazungu walioanzisha shule ya kwanza Tanganyika na kanisa. Luteni Kanali Mhina aliyelitumikia Taifa kwa muda mrefu kama mwanajeshi, na baadaye kuwa Mbunge wa Muheza kutoka mwaka 1990 hadi 1995,anasema harakati za kuanzisha shule katika kijiji hicho zilitokana na Wamishenari waliokuja Afrika Mashariki kutoka Ulaya kwaajili ya kueneza dini ya kikristo tangu miaka ya 1770. Anawataja baadhi ya Wamishenari hao kuwa ni pamoja na David Livingstone,Charles Mackenzie, William Tozer na Edward Steer. Anasema harakati hizo zilianzia tangu visiwa vya Zanzibar mwaka 1863 ambako pia walikomesha biashara ya utumwa na kuanza ujenzi wa kanisa la Anglikana la Mkunazini Zanzibar kwa miaka 10 tangu mwaka 1873. Anasema wakati huo kulikuwa na shule iliyoanzishwa Zanzibar maeneo ya Kiungani na Kiinua mguu na Askofu William Tozer mwaka 1869. Hata hivyo, anasema shule hiyo haikuwa rasmi na ilikuwa ikifundisha elimu ya dini kwa watumwa waliokombolewa.

Wednesday, 21 November 2012

HILI LINAWAHUSU WANAWAKE ZAIDIII SOMA…

Jee unajua kuwa kufanya kazi usiku ni hatari kwa akina mama? Na inaweza kusababisha kifo? Utafiti uliofanywa na madaktari nchini Uingereza umegundua kuwa wanawake wanaopendelea kufanya kazi usiku wanahatari ya kupatikana na sartani ya matiti-breast cancer. Katika kichwa cha Kazi za usiku zinasababisha vifo 500 kila mwaka nchini Uingereza utafiti hunasema shift za usiku ni hatari kwa akina amma. Dr Lesley Rushton,wa Imperial College Mjini London anasema Mawanamke akifanya kazi ya usiku kwa wastani ya siku tatu kwa wiki kwa miaka sita - anakaribisha kansa ya matiti. Kufanya kazi usiku au kukosa usingizi kwa akina mama kunatatiza utengenezaji wa homoni ya ya MELATONI, hii ni chembechembe inayosaidia usingizi na hii inasadikiwa kuwa na uwezo wa zuia kansa.

Tambua Madhara ya Sindano za uzazi wa mpango....

UTAFITI umebaini kuwa sindano za uzazi wa mpango zinachangia kasi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi,kwa kuwa zina vichocheo vingi ambavyo vinahuisha virusi vya Ukimwi katika nyumba ya uzazi na kuvipa nguvu ya kusambaa. Inaelezwa kuwa walio katika hatari zaidi ya maambukizi hayo ni wanawake walioko katika ndoa kwa kuwa ndiyo wanaotumia zaidi sindano hizo. Utafiti huo uliofanywa na wanasayansi wa Marekani na kuripotiwa na gazeti la The Guardian la Uingereza, umebaini kuwa wanawake wanaotumia sindano za uzazi wa mpango wapo katika hatari mara mbili ya kupata maambukizi ya Ukimwi au kuwaambukiza wenzi wao, kuliko wengine. Katika utafiti huo uliofanywa katika nchi saba zinazoendelea barani Afrika ikiwamo Tanzania, wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Washington,walipendekeza ushauri zaidi utolewe kwa wanandoa kabla mtu hajajiingiza kwenye matumizi ya sindano kama njia ya kupanga uzazi. Utafiti huo ulifanyika kwa wanandoa 3,790 kutoka nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Zimbabwe, Uganda, Kenya, Rwanda na Botswana, ulichapishwa kwa mara ya kwanza katika Jarida la Afya la Lancet kabla ya kunukuliwa na gazeti la The Guardian. Utafiti umebaini pia kuwa zaidi ya wanawake 140 milioni duniani,wanatumia njia mbalimbali za uzazi wa mpango, huku wanandoa wengi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanaoishi na VVU wakichagua kutumia sindano kama njia ya kuzuia mimba zisizotarajiwa. Wanasayansi hao walikusanya taarifa kati ya wanandoa 3,790 ambao mmoja wao anaishi na VVU na mwenza wake akiwa hana maambukizo. Aidha wanawake ambao wanaishi na VVU na wanatumia sindano hizo pia,walikuwa katika hatari zaidi ya kuwaambukiza wenzi wao. Vipimo vilionyesha kuwa sindano hizo ambazo zina vichocheo ambavyo vinavipa nguvu virusi ndani ya nyumba ya uzazi (cervix). Imeelezwa kuwa njia za uzazi wa mpango zinazohamasishwa zaidi na kupendwa zaidi na wanawake ni sindano, ambazo wanawake wanasema kuwa zinadumu kwa muda mrefu na zinaweza kutumika bila ya ruhusa au mume kufahamu. Kiongozi mkuu wa utafiti huo Renee Heffron wa Chuo Kikuu cha Washington,alisema sindano za uzazi wa mpango zina vichocheo vingi ambavyo huvihuisha vijidudu vya Ukimwi katika nyumba ya uzazi na kuvipa nguvu ya kusambaa. Mwanasayansi mwingine, Charles Morrison wa Kituo cha Afya cha Durham, nchini Marekani alisema uhamasishaji wa matumizi ya sindano za uzazi wa mpango unachochea maambukizi zaidi katika nchi za Jangwa la Sahara. Na ameshauri nchi zinazoendelea kuacha matumizi ya njia za uzazi wa mpango zenye vichocheo, ili tupunguze maambukizi. Alivitaka vituo vya afya vitoe ushauri kwa wanawake kutumia kondomu badala ya sindano au vidonge. Mara nyingi watu wanaotumia vidonge, wengi si wanandoa, mtu anayemeza vidonge vya kuzuia mimba anaogopa zaidi mimba si Ukimwi. Huchoche hamu ya mapenzi. Mfamasia katika Kitengo cha Dawa kwa watu wanaoishina VVU katika Hospitali ya Amana Christopher Masika,alisema anaafiki kuwa sindano na hata vidonge vinaweza kuwa ni sababu inayochochea maambukizi kwa sababu ya uhuru. Kwa sababau Mtu anapotumia sindano huwa huru kufanya ngono,kwa kuwa hana hofu ya mimba hicho kinaweza kumfanya apate maambukizi kwa urahisi, tofauti na anapotumia kondomu. Amesema wapo baadhi ambao wakitumia sindano hizo vichocheo vinawafanya wapate hamu zaidi ya kufanya mapenzi, hivyo huanza kutembea na wanaume wengine.

Monday, 5 November 2012

VYAKULA TUNAVYOKULA VINAVYOTUMALIZAAaaaa

Tukumbuke kwamba uzima wa mtu unategemea sana kinga aliyonayo mwilini,kinga ambayo hujengwa na ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vya aina mbalimbali. Kwa namna ambavyo Mungu ametuumba, mwili unapaswa kujilindi wenyewe dhidi ya maradhi ya kila aina. Ukiwa na kinga imara ya mwili siyo rahisi kuugua mara kwa mara. Magonjwa yanayojitokeza haraka pale kinga ya mwili inapokuwa chini, ni pamoja na kuugua malaria mara kwa mara, kifua kikuu, kutokwa na majipu, kutokwa uvimbe wa ajabuajabu katika mwili, kupatwa na mkanda wa jeshi, kupatwa na saratani na magonjwa mengine ya maambukizi. Huo ni mfano wa kundi moja la magonjwa ya maambukizi, lakini hata magonjwa mengine hatari kama shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, magonjwa ya viungo, kisukari, macho, na mengine mengi, huwa ni matokeao ya ulaji wa vyakula visivyo sahihi au uachaji wa ulaji vyakula muhimu.
CHANZO CHA KUSHUKA KWA KINGA Ili uwe na kinga imara ya mwili, ni lazima uwe unakula mlo kamili unaojumuisha matunda, mboga za majani, nafaka na vyakula vingine vya asili, kwa sababu kila unachokula kina faida yake mwilini. Lakini siyo tu kula chochote kinachoitwa ‘chakula’, bali ule kilichosahihi na kilichosahihi. Katika maisha tunayoishi sasa, hasa mijini, idadi Kubwa ya watu hawali kabisa vyakula sahihi, badala yake wanakula vyakula ambavyo si tu ni hatari kwa afya zao, bali pia hudhoofisha kinga ya asili ya mwili na hivyo kuufanya mwili kubaki dhaifu na unaoweza kupatwa na ugonjwa wowote. Chanzo kikuu cha kushuka kwa kinga ya mwili kunasababishwa na ulaji wa vyakula visivyo sahihi ambavyo ndivyo vinavyopatikana kwa wingi kila mahali, hasa sehemu za mijini. Vyakula visivyofaa ndivyo vinavyotangazwa na kunadiwa kwenye vyombo vya habari kuwa bora. VYAKULA HATARI VINAVYOLIWA KILA SIKU Kuna orodha ndefu sana ya vyakula hatari ambayo huliwa kila siku, kuanzia asubuhi hadi jioni. Vyakula hivi yumkini huliwa kwa takriban maisha yote ya mtu na huonekana ni vya kawaida.Baadhi ya vyakula hivyo ni kama vile unga wa ugali, mkate, chips na juisi. UNGA WA UGALI Unga wa ugali unaotumiwa na watu wengi nchini ni sembe nyeupe. Chakula kikuu katika kaya nyingi zinazotumia ugali kama mlo wa kila siku huwa ugali mweupe uliotokana na mahindi yaliyokobolewa na kusafishwa, kisha kusagwa na kutoa unga safi mweupe. Kwa mtizamo wa macho na ladha ya mdomoni, wengi wanaamini kuwa ugali wa aina hii ndiyo mzuri na unaotakiwa kuliwa. Ulaji wa ugali wa aina hii hauna faida yoyote mwilini, kwani hauna virutubisho,kwa sababu vilishaondolewa vyote wakati wa kukoboa. Virutubisho muhimu vya muhindi viko kwenye kiini chake, hivyo unapokiondoa unakuwa umeondoa lishe muhimu. Ndiyo maana hata panya hawali mahindi yaliyokobolewa. Kwa faida ya afya zetu na kwa ajili ya kuimarisha kinga ya miili yetu, sote tunatakiwa kula ugali wa dona, mtama au ulezi kabla hata ya kuugua. Vyakula hivi ni muhimu sana na siyo vya kimasikini kama ambavyo watu wengi wanadhani. Kwa bahati mbaya, upatikanaji wa unga wa dona umekuwa mgumu na ghali kuliko sembe nyeupe, hivyo kuwafanya watu wengi kukimbilia sembe nyeupe ambayo inapatikana kirahisi kila kona ya nchi na kwa bei nafuu. Kwangu mimi naliona tatizo hili ni la kitaifa na kisera. Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ilipaswa kutoa elimu ya kutosha ya kuelezea madhara yatokanayo na ulaji wa sembe nyeupe kisha kuweka sera itakayokataza uzalishaji wa kibiashara wa sembe nyeupe kama ilivyo sasa. Sera ya namna hii ingeokoa maisha na afya za Watanzania wengi wanaoteketea kila situ kutokana na ugonjwa wa kisukari. Naamini kaya nyingi nchini hazijui kabisa kama ugali utokanao na sembe nyeupe wanaokula kila siku iendayo kwa Mungu, una madhara kiafya. Ni vigumu kuzieleza na zikakuelewa familia ambazo kwa maisha yao yote zimekuwa zikiamini kwamba kula ugali mweupe ndiyo kitu bora. Serikali ilipaswa kuliangalia suala hili na kuona kama janga la kitaifa, ilipaswa kuanzisha kampeni maalum ya kutoa elimu kuhusu vyakula na lishe kwa njia mbalimbali, zikiwemo za matangazo redioni na kwenye televisheni.
ULAJI WA MATUNDA NA MBOGA Hakuna kitu muhimu kwa mwili wa binadamu kama kujenga kinga ya mwili. Mwili unapokuwa na kinga imara, si rahisi kuugua magonjwa ya ajaba. Miongoni mwa kazi nyingi za matunda na mboga za majani, ni pamoja na hiyo kazi ya kujenga mwili na kuujengea uwezo wa kujikinga wenyewe. Pamoja na umuhimu huo, ni watu wachache sana hula matunda na kuyachukulia kama sehemu ya milo yao ya kila siku. Watu wengi hula matunda au mboga za majani ‘kwa bahati mbaya’, huona siyo chakula muhimu sana. Hili ni kosa kubwa miongoni mwa makosa mengi yanayofanywa na watu katika masuala ya afya. Matunda yanatakiwa kuliwa kila siku na kwa wingi, vivyohivyo mboga za majani. Unapoacha kula matunda na mboga za majani za aina mbalimbali, jua unaukosesha mwili wako kinga dhidi ya maradhi yanayoweza kujitokeza mwilini. VYAKULA HIVI NDIYO VINAVYOTUMALIZA
Vyakula tunavyotakiwa kuvila, hatuvili tena na pengine upatikanaji wake ni wa shida, hivyo tunalazimika kula vilivyopo licha ya kuwa vina madhara kwa afya zetu. Hali hii imeongeza idadi ya wagonjwa na magonjwa sugu. Chakula kikuu cha mijini ni chips, kuku, mayai, soda, juisi za makopo au paketi, nyama choma na pombe. Pia kuna mkate mweupe, maandazi na chapati. Vyakula hivi huliwa kila siku, lakini ukivichambua utagundua havina faida yoyote mwilini zaidi ya kuingia na kutengeneza maradhi.
CHIPS Chips ambayo kwa kawaida hutengenezwa kutokana na viazi mviringo na kukaangwa kwenye mafuta, ni chakula kinachotakiwa kuliwa kwa kiasi kidogo na kwa nadra sana, kwa sababu kiko kwenye kundi la vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo huliwa kwa uchache sana.Lakini hali halisi ni kinyume chake. KUKU Kwa kawaida, kuku wengi wanaotumika kwenye biashara ni kuku wa kizungu. Nyama ya kuku hawa haina virutubisho sawa na kuku wa kienyeji. Hii inatokana na ukweli kwamba kuku wa kizungu hulishwa madawa mbalimbali ya kuwakinga na magonjwa na hulishwa vyakula vilivyochanganywa madawa ili wakue upesi. Kwa mazingira hayo, nyama itokanayo na kuku wa aina hii haiwezi kuwa bora. Kiasili kuku huishi mazingira huru kwa kula vyakula ambavyo hujenga na kuukinga mwili wake dhidi ya magonjwa mbalimbali, kuku wa aina hii ndiye anayefaa kuliwa na kuleta faida ya nyama ya kuku inayokusudiwa. MAYAI Halikadhalika, mayai yanayopatikana kwa wingi mijini ni yale yatokanayo na kuku wa kufuga. Kiasili, mayai ya kuku wa kufuga, hayawezi kuwa sawa na mayai yatokanayo na kuku wa kienyeji. Huhitaji kuwa mwanasayansi kuona tofauti kati ya yai la kuku wa kienyeji na kuku wa kufuga, kwani mayai hayo yakipikwa huwa tofauti kwa ladha na hata rangi. Ni ukweli ulio wazi kuwa kuku wa kufugwa hulishwa vyakula vya kutengeneza ambavyo ndani yake huwekwa kemikali na madawa mbalimbali, wakati kuku wa kienyeji hula vyakula asili kwa kujitafutia wenyewe na mazingira wanayoishi ndiyo yanayowafanya wawe tofauti na bora. Hivyo ni dhahiri kwamba mayai tunayokula ya kuku wa kizungu yana madhara zaidi kuliko faida mwilini. SODA Moja ya vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa na watu wengi ni pamoja na soda. Matangazo mengi ya biashara yanafanyika kutangaza kinywaji cha soda na kuonesha kuwa ni kinywaji ambacho hakina madhara kabisa kwa mtumiaji. Kwa matangazo hayo na kampeni hizo, familia nyingi zimeamini kuwa soda ni kinywaji bora na hata watoto wetu wamerithishwa imani hii. Lakini kwa upande wa pili wa kinywaji hiki, siyo kinywaji salama kama ambavyo imekuwa ikielezwa. Siwezi kusema moja kwa moja kuwa mtu huruhusiwi kabisa kunywa soda kama vile ni sumu, lakini watu walitakiwa kuelimishwa na kuelezwa madhara ya kupenda kunywa soda na athari anazoweza kuzipata mtu kiafya. Naamini tahadhari inayotolewa kwa wanywa pombe, hata kwa wanywa soda ilipaswa kutolewa pia. Utafiti unaonesha kuwa soda, pamoja na vikorombwezo vingine, huwekwa sukari nyingi kiasi kisichopungua vijiko sita katika chupa moja. Kiwango hicho cha sukari ni kingi zaidi ya mara tano ya kile kinachoruhusiwa kwa mtu kutumia kwa siku. Na madhara ya sukari mwilini ni mengi, yakiwemo ya kudhoofisha kinga ya mwili na viungo kwenye sehemu za maungio na pia huongeza uzito wa mwili. Ukitaka kujua soda ina madhara kiafya, fanya utafiti binafsi na utagundua haya ninayoyaandika. Kunywa soda zisizopungua tatu kwa muda mfupi, kisha lala usiku kama kawaida halafu wakati wa kuamka asubuhi, usikilize mwili wako.Utaamka ukiwa na maumivu mwili mzima, utajihisi uchovu, hasa sehemu za maungio, mfano wa mtu aliyefanya mazoezi mazito au kazi nzito siku iliyopita. Hiyo ni kutokana na kuingiza kiwango kingi cha sukari mwilini.
JUISI Katika hali ya kawaida, juisi ni kinywaji baridi kisicho na kilevi wala madhara kwa mnywaji. Lakini utakuwa sahihi ukizungumzia juisi zilizotengenezwa kwa matunda halisi bila kuongezewa vitu vingine. Katika zama hizi, hali iko tofauti, juisi nyingi tunazodhani ni vinywaji baridi visivyo na madhara kwa afya zetu na za watoto wetu, hali haiko hivyo. Juisi nyingi zinazouzwa kila sehemu ni feki. Ni jambo lakusikitisha kuona jinsi binadamu anavyojaribu kushindana na Mungu kwa kutengeneza vitu vinavyofanana na vile alivyoumba Mwenyezi Mungu kwa ajili yetu. Juisi nyingi hutengenezwa kwa kuchanganya maji, sukari na rangi zilizotengenezwa kwa kemikali mbalimbali zikiwemo zenye ladha ya matunda. Juisi za aina hii ndiyo nyingi na zinapatikana kila kona ya nchi hii, waathirika zaidi wakiwa watoto wetu ambao hupenda kunywa kwa kufuata utamu wa sukari nyingi zilizowekwa na ladha za matunda. Utafiti umeonesha kemikali (Additives) zinazowekwa kwenye vinywaji hivi, hudhoofisha kinga ya mwili na huwa chanzo cha magonjwa ya saratani na mengine hatarishi. Nakusihi kuacha kunywa kabisa juisi hizo na usimpe mwanao, unamuua. Ukiacha hizo juisi zinazotengenezwa kwa kutumia kemikali ‘mwanzo mwisho’, kuna juisi zingine zinazodaiwa kutengezwa kutokana na matunda, zipo za ‘machungwa’, nanasi’, ‘pasheni’, n.k. Yapo makampuni pia yanayojitapa kutengeneza juisi zao asilimia 100 kutokana na matunda na kwamba hakuna kinachoongezwa kingine. (100% fruit, No sugar added au No additives, huandika hivyo kwenye maboksi yao au makopo wanayoweka juisi. Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa makampuni mengi yanadanganya walaji. Kwa sababu siyo kweli kwamba hawaongezi kitu kingine katika utengenezaji wa juisi zao za matunda. Imejulikana kuwa huweka vitu vya kufanya juisi ya kwenye boksi au chupa ikae kwa muda mrefu bila kuharibika, halikadhalika huweka vitu vya kuifanya juisi hiyo kuwa na ladha moja. Acha nikupe mfano. Katika hali ya kawaida, ukichuma machungwa matano ya mti mmoja, lazima yatakuwa na ladha tofauti, yote hayawezi kuwa na ladha sawa japo yote yanatoka mti mmoja. Kwa maana hiyo, kama ukitengeneza juisi kwa kutumia machungwa yaliyochumwa kutoka miti tofauti, ladha ya juisi lazima itatofautina. Lakini utashangaa kuona ladha ya jusi za maboksi zote zinafanana. Wanachofanya ni kuweka ladha moja kwenye utengenezaji wa juisi zao kabla ya kupeleka kwa mlaji. Halikadhalika, juisi ukishaitengeneza, haiwezi kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Kwa hiyo, ili kuifanya juisi hiyo iweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika, lazima iwekewe kemikali ya kuihifadhi isiharibike.Kwa kuongezewa vitu hivyo, hata kama Kwa maelezo hayo, hatushauriwi sana kunywa juisi hizo ‘ready made’ kwa sababu zimekosa uhalisia, kwani zina madhara kwa afya zetu, licha ya maelezo na matangazo mazuri tunayopewa na watengenezaji. Badala yake tutengeneza juisi majumbani mwetu wenyewe kwa kutumia matunda halisi ili kupata faida katika miili yetu. Jiepushe na matumizi ya sukari nyingi katika juisi unayoitengeneza mwenyewe, kwani kwa kufanya hivyo utakuwa unaiharibu, weka sukari kidogo sana ikiwezekana acha kabisa.

HEBU TAFAKARI HAYA KWA KINAaaaa.....

1. Maisha yako yanaweza kubadilishwa kwa muda mfupi na mtu hata usiemjua. 2. Watu wenye furaha pengine hawana kila kitu cha kuwapa furaha ila kile kidogo walichonacho hukipa maana ya kukifurahia.3. Wapenzi wawili wanapogombana haimaanishi hawapendani,vivyohivyo wasiogombana haimaanishi wanapendana. 4. Unaweza kufanya jambo fulani la muda mfupi lakini likakunyima furaha milele .5. Unapoagana na uwapendao waache na maneno mazuri pengine inaweza kuwa mara yako ya mwisho kuwaona. 6. Inaruhusiwa kuwa na hasira ila haimaanishi uwe katili.7. Ukomavu wa mtu huja kutokana na changamoto alizozipitia kwenye maisha na kujifunza kupitia changamoto hizo na sio umri aliouongeza. 8. Wakati mwingine inatosha kusamehewa na wengine,ifike mahali ujifunze kujisamehe mwenyewe. 9. Sio lazima uwe na kiherehere cha kujua siri flani pengine kuijua kunaweza kubadili maisha yako milele. 10. Watu wawili wanaweza kutazama kitu kimoja lakini kila mmoja akaona tofauti