Hii inamaanisha kuwa bei ya tembe moja ya dawa inayotumika
kupunguza makali ya ukimwi itapanda kutoka dola $13.50 hadi $750.
Kampuni hiyo inayoitwa Turing Pharmaceuticals, imelaumiwa na
washika dau wa maswala ya Ukimwi kwa kuongeza bei ya dawa hiyo ya Daraprim,
ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha uwezo wa mwili wa mgonjwa
aliyeathirika kupigana na maambukizi mapya.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Martin Shkreli, amenukuliwa
akisema kuwa faida itakapatikana baada ya mauzo ya dawa hiyo, itasaidia
kugharamia utafiti wa dawa mpya na zenye ubora zaidi.
Tembe moja ya dawa hiyo ya Daraprim inagharimu dola moja
pekee kuitengeneza.
Hata hivyo
bwana Martin anasema kuwa bei hiyo haijumuishi gharama ya kunadi dawa hiyo wala
usambazaji wake, ingawa gharama imeimarika maradufu katika miaka ya hivi punde.
Daktari Wendy Armstrong kutoka muungano wa wauguzi nchini Marekani
HIV Medicine Association, amekashifu sababu zilizotolewa kwaajili ya nyongeza
hiyo kubwa ya bei ya dawa hiyo.
Katika siku za hivi karibuni dawa za kupunguza makali ya
saratani, zinagharimu dola laki moja ilhali gharama yake asili inaweza
kugharimu dola nusu milioni.
0 comments:
Post a Comment