Tuesday, 8 September 2015

Je umeambukizwa Nomophobia..? Soma utafiti

Utafiti wa hivi karibuni uliowachunguza wanafunzi 1000 Korea Kusini, umebaini kuwa asilimia 72 ya watoto wanapata simu wakifikia umri wa miaka 11 au 12.

Aidha kwa Wanafunzi hao huzitumia simu hizo za kisasa kwa karibu saa tano na nusu ya muda wao kwa siku.
Matokeo yake ni kuwa asilimia 25 ya watoto ama mmoja kati ya wanafunzi 4 ametajwa kuwa na uraibu wa simu hizo.
Nchi ya Singapore karibu kila raia anamiliki simu ya kisasa ya mkononi, raia huko ni milioni sita pekee.
Kwa sababu ya uraibu huu nchi hiyo imejenga kiliniki maalum ya kuwashugulikia walio na tatizo la Nomophobia, yaani kuipenda simu kupindukia.

Lakini hata China wamefungua kiliniki yao kama hiyo ya Singapor kwa ajili ya kutibu Nomophobia, yaani kuipenda simu kupindukia.

0 comments:

Post a Comment